FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,060
Habari!
Israel imetangaza Alhamisi kuwa inashirikiana na Marekani katika mpango wa uundaji wa mfumo mpya wa ulinzi wa anga dhidi ya makombora ya balistiki unaojulikana kama Arrow-4 ambao unajumuisha kizazi kijacho cha vizuizi (interceptors) ambao utachukua nafasi ya mfumo uliopo wa Arrow-2 kwa miongo kadhaa ijayo, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Israel.
Hili linafuatia ikiwa ni siku moja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusiana na masuala kadhaa yakiwemo usalama pamoja na ushirikiano kati ya nchi hizo.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Biden aliandika,
Sekta ya ulinzi ya Israel mpaka sasa imeunda aina mbalimbali za mifumo ya ulinzi wa anga na makombora, ikiwemo Arrow-3, Iron Dome, David Sling pamoja na Barak 8 sanjari na mifumo ya kisasa ya rada. Mifumo hiyo mbalimbali imeundwa kukabiliana na hatari mbalimbali za anga kuanzia roketi hadi makombora ya balistiki na yale ya kuvinjari (cruise).
Mifumo iliyopo ya Arrow: Arrow-2 pamoja na Arrow-3 ingali ikifanya kazi kama sehemu ya mfumo wa safu nyingi ama kwa lugha nyingine, multi-layered system, wa kuzuia makombora kutoka angahewa (atmosphere) na anga za mbali (space).
Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz alisema kuwa, mpango huo kushirikiana na Marekani ambao utekelezaji wake umeanza rasmi utapelekea maendeleo makubwa ya kiteknolojia katika kukabiliana na hatari za kivita na mashambulizi ya makombora katika eneo la Mashariki ya Kati na kwingineko duniani.
Benny Gantz alisema,
Wizara ya Ulinzi pia ilisema kuwa, kampuni ya Israel ya masuala ya anga: uzalishaji na uundaji wa mifumo ya usafirishaji ya anga, Israel Aerospace Industries, ndiye mkandarasi mkuu katika mradi huu wa Arrow-4. Kampuni hiyo pia imehusika katika uzalishaji wa mifumo mingine ya ulinzi wa anga ya Arrow. Kampuni nyinginezo: Boeing ya Marekani pamoja na Elbit Systems ya Israel pia ni sehemu ya mradi huu wa Arrow.
Kwa taarifa zaidi kuhusiana na hili, waweza pitia katika vyanzo zifuatavyo:
1) Reuters | Israel says developing new Arrow-4 ballistic missile shield with U.S.
2) Defense News | Israel and US begin Arrow-4 development
3) Sputnik International | Defence Ministry Announces Joint Israeli-US Project to Create New Ballistic Missile Shield

I spoke today with @IsraeliPM Netanyahu and affirmed the United States' steadfast commitment to our ally Israel's security. Our teams are in constant touch to strengthen U.S.-Israel strategic cooperation on all regional security issues, including Iran.
Sekta ya ulinzi ya Israel mpaka sasa imeunda aina mbalimbali za mifumo ya ulinzi wa anga na makombora, ikiwemo Arrow-3, Iron Dome, David Sling pamoja na Barak 8 sanjari na mifumo ya kisasa ya rada. Mifumo hiyo mbalimbali imeundwa kukabiliana na hatari mbalimbali za anga kuanzia roketi hadi makombora ya balistiki na yale ya kuvinjari (cruise).
Mifumo iliyopo ya Arrow: Arrow-2 pamoja na Arrow-3 ingali ikifanya kazi kama sehemu ya mfumo wa safu nyingi ama kwa lugha nyingine, multi-layered system, wa kuzuia makombora kutoka angahewa (atmosphere) na anga za mbali (space).
Waziri wa Ulinzi wa Israel Benny Gantz alisema kuwa, mpango huo kushirikiana na Marekani ambao utekelezaji wake umeanza rasmi utapelekea maendeleo makubwa ya kiteknolojia katika kukabiliana na hatari za kivita na mashambulizi ya makombora katika eneo la Mashariki ya Kati na kwingineko duniani.
Benny Gantz alisema,
Along with the development of vital offensive capabilities, the defense establishment is constantly working to defend Israel's skies against ballistic threats through the ongoing development of its multi-layered [missile defense] array. The development of Arrow-4 together with our American partners will result in a technological and operational leap forward, preparing us for the future battle field and the ever-evolving threats in the Middle East and beyond.