Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,884
- 5,235
- Thread starter
- #21
Kwa serikali ya Israel dini kwao sio jambo kabisa, what concern them is the Map of the world.
==========
Mzozo wa Israel na Palestina: Kwanini jamii ya Wakristo itaangamia Jerusalem iwapo mzozo huo utaendelea
18 Mei 2021, BBC.
Chini ya Juma moja , mzozo kati ya Israel na Palestina umeongezeka na kusababisha ghasia chungu nzima.
Umewawacha watu 127 wakiwa wamefariki na mamia kujeruhiwa katika mashambulizi ya pande zote mbili.
Ni hali ngumu zaidi katika kipindi cha miaka mitano , na Umoja wa mataifa unahofia kuzuka kwa vita vya kiwango cha juu.
Na kati ya mzozo huo , jamii za wachache wanatathmini jinsi mzozo huo ambao haujatatuliwa kwa miaka 70 unahatarisha uwepo wao.
Wakristo wa Palestina waliohamia katika eneo hilo na ambao wanawakilisha asilimia moja ya idadi ya watu katika eneo hilo , wanasema kwamba njia mbadala iliopo ni kuondoka .
''Sisi sio Wakristo tu. Tuko zaidi ya Wapalestina Waarabu na kila kitu kinachofanyika hapa kinatuathiri moja kwa moja'' , anasema Bandak Saleh, Mkristo wa Orthodox anayeishi Bethlehemu katika eneo la West Bank alipozungumza na BBC Mundo.
Iwapo mzozo huo hautatatuliwa , hakutakuwa na Wakristo katika ardhi ambayo Yesu alizaliwa, anasema
Wengi wa Wakristo wanaoishi Jerusalem ni Wapalestina.
BBC Mundo ilizungumza na baadhi ya viongozi wa makanisa ya Kikristo wanaoishi katika eneo la Wapalestina kubaini ni vipi wanauona mzozo huo, kiwango cha ghasia na hatma yao katika eneo hilo.
1.Itakadi kali zinavujisha damu mji mtakatifu
Kwa sasa , idadi ya Wakristo katika eneo la Palestina ni 50,000 ambayo ni asilimia moja pekee, iliosambaa katika mji wa Bethlehem, Ramallah na Jerusalem, mbali na wale wanaoishi ukanda wa Gaza.
Kati ya wote ,asilimia 48 inamilikiwa na watu wa kanisa la Orthodox Ugiriki , asilimia 38 kanisa Katoliki na iliosalia ikimilikiwa na waumini wa kanisa la Protestant, Presbyterian na Orthodox wenye sheria tofauti kutoka Syria na Armenia,
Katika miji hiyo ni baadhi ya vivutio vya mahujaji kwa dini zao tofauti, maeneo ambayo Yesu alizaliwa , kuhubiri na kufariki , kulingana na Biblia na tamaduni za Kikristo.
''Kwa viongozi wa Kikristo katika eneo hilo, madai yaliopo ni kwamba vitendo vya serikali ya Israel ni miongoni mwa majaribio yalioshinikizwa na mawazo ya itikadi ambayo yanawanyima watu haki ya kuishi katika makazi yao," kama anavyozungumza Askofu wa kanisa katoliki mjini Jerusalem Pierbatista Pizzaballa.
''Na hilo linaliza roho za mji huo mtakatifu'', anaongezea.
Kwa upande wake ,katibu mkuu wa baraza la makanisa katika eneo la mashariki ya kati Michel E, Abs anasema kwamba kuna madhara ya moja kwa moja: Kila mzozo , vita na mgogoro wa kisiasa kila mara husababisha watu kuwachwa bila makao na kwamba watu ni sharti waishi katika eneo wanaloishi, aliambia BBC Mundo.
Kwake yeye , kwa kuwa Wakristo ni wachache , tisho hilo linawaweka katika hatari ya kutoweka iwapo mzozo huo utaendelea.
''Wakristo Waarabu ambao ni lazima watoroke, hawana uwezo sawa ambao Waarabu Waislamu wanao ambao ndio wengi. Hali hiyo inaweza kuangamizi jamii hiyo ambayo imeishi katika eneo hilo la Palestina kwa karne nyingi'', anasema katibu wa baraza hilo.
Hatahivyo tisho hilo haliishi.
''Huwezi kuimarika kimaisha iwapo kuna watu ambao wanataka kukuondoa katika eneo unaloishi , kukata miti ambayo umepanda nyumbani kwako , ama iwapo hawezi kukuacha utembee ukiwa huru'', anasema.
Kitu muhimu kwa Wakristo ni usaidizi waliopokea kutoka kwa Wakristo Wapalestina wanaoishi nje ya eneo hilo - katika mataifa mengine na ambao wamesaidia kuimarisha mtandao wa usaaidizi ulioanzishwa na vituo vya kijamii hususan katika eneo la West Bank.
Jukumu la viongozi wa Kikristo walilochukua limesaidia katika eneo la chini , wakisaidia jamii yao , kupitia parokia , kwa njia ya kidini licha ya kwamba wanaofaidika ni Wakristo au sio, anasema.
"Jamii ya Wakristo ina uzito mkubwa katika eneo hilo , lakini ni ndogo : Mariano Aguirre , mtaalamu wa mambo ya mashariki ya kati anasema.
Mzozo huo unawaathiri wale wote wanaoishi Jerusalem katika eneo kwa jina mji wa kale na eneo la mashariki, ambapo Wapalestina huwachwa bila makao mara kwa mara na ambao uhisi wananyanyaswa na walowezi wa Kiyahudi.
Jamii ya Kikristo hususan huathiriwa kwasababu mbili .
Moja ya sababu za unyanyasaji wa mara kwa mara unaofanyiwa Wakristo wa kanisa la Orthodox na wawakilishi wao wa kidini na walowezi wa KIyahudi.
Sababu nyengine ni kwamba idadi ya Wakristo 16,000 inayoishi Jerusalem 13,000 ni Wapalestina .
Jamii ya Wakristo inayoishi Jerusalem ni ndogo . Ina uwezo mkubwa wa kidini lakini uwezo wake wa kushawishi kisiasa katika mgogoro wa Israel na Palestina ni mchache .
2. Iwapo kuna mzozo hakuna uchumi
Mjini Jerusalem , utalii na biashara imeathiri shinikizo za Israel kuchukua kwa nguvu hoteli zilizopo katika mji huo wa kale ambazo zinamilikiwa na makanisa ya Wakristo.
Walid Dajani anamiliki hoteli ya Imperial, ambayo hufanya kazi ndani ya jumba ambalo humilikiwa na kanisa la Ugiriki la Orthodoz na ambalo lipo ndani ya maeneo matakatifu ya mji huo.
Dajani anasema kwamba ameshuhudia shinikizo kutoka kwa makundi ya Israel yenye itikadi kali kuondoka maeneo hayo na kupeana mali yake.
Limekuwa tatizo kubwa.
Jumba hili limemilikiwa na kanisa la Orthodox kwa karne kadhaa na kutokana na maamuzi ya mahakama ambayo hatuyaelewi , wanakaribia kupoteza udhibiti huo, Dajani aliambia BBCMundo.
3. " Hatuwezi kwenda kanisani "
Saleh Bandak ameripotiwa kukamatwa . na amehudumu siku kadhaa jela Israel. Baada ya miaka kadhaa ya uanaharakati wa kisiasa , sasa ameingia ktika biashara ya chakula .
Anaishi Bethlehem ambapo anamiliki mgahawa karibu na kanisa la Nativity , moja ya vituo vikuu vinavyovutia katika ardhi hiyo takatifu.
''Mimi ni Mkristo wa Orthodox na mara nyingi , ninapotaka kwenda kusali katika hekalu la Maria Magdalina ambalo ni mojwapo ya makanisa yaliopo ambayo hayapatikani Jerusalem , hawataki kuniruhusu nipite, siwezi kupita'', Saleh anaambia BBC Mundo.
Na kwake yeye hatua hiyo inaweza kuwa na thari katika siku za mbeleni , hadi kufikia kiwango ambacho kutakuwa hakuna Wakristo tena katika eneo la Wapalestina.
''Hakuna mtu anayetaka kuishi hivi. Watu wanataka kuishi kwa utulivu na amani, iwapo wanataka kwenda kusali ambacho ni kitu cha kila siku , wanapaswa kufanya bila kulazimika kutoa stakhabadhi wanapokwenda kanisani'', anadai
BBC
View attachment 1790302View attachment 1790303View attachment 1790305View attachment 1790304