Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Vyombo vya habari vya Ulaya vilikuja na taarifa kuhusu bwana mdogo Israel Olatunde ambaye ni raia wa Ireland kwa kuzaliwa na moja ya mwanamichezo ambaye anajitazama kama raia wa Ireland, huku pia akiwakilisha nchi yake kwenye mchezo wa riadha kama Irish man.
Wazazi wake ni Wanaijeria kwa asili zao ingawa waliondoka na kuhamia Ireland mwaka 1999 na Israel amezaliwa Ireland mwala 2002 na kukulia huko huko.
Sasa kama kawaida yetu kuwatengeneza label raia wenye damu za kiafrika haswa wale waliofanikiwa, basi Wanaijeria wameanza kumuita Israel kuwa sio raia wa Ireland kwa maana ya kwamba sio mzungu na kudai kuwa hakuna mtu mweusi ambaye ni Irish.
Tunaposhindwa kuandaa watu wetu ambao tunawaona wakijitahidi kwenye michezo sio busara kutamani mafanikio yao endapo wakiwa sio tena raia wa nchi husika.
Israel Olatunde sio mnaijeria tena bali ni Irish, na tuheshimu hilo, sasa nyota ya dogo imeanza kung'aa watu wameanza kutafuta nafasi ya Nigeria kuchukua sifa ilihali waliomsaidia sio Wanaijeria bali ni Ireland.