Achana na ile misaada ya Marekani ya dola bilioni 4 kila mwaka (trilioni 10) ambayo huwa sio cash, huwa ipo katika mfumo wa silaha na vifaa
Dola bilioni 271 ndio bajeti yao Israel, ni shilingi trilioni 700 kasoro vichenchi kidogo
Mapato mengi ni kutokana na teknolojia, karibia kila kampuni kubwa ya teknolojia kama iphone, samsung, chip za computer na simu, dell, hp, intel, n.k. wana ofisi zao nchini Israel, wanawalipa waisraeli kuwabunia na kuwaboreshea teknolojia, kule china huwa ni mambo ya viwanda tu, Marekani na Ulaya huwa ni ofisi kuu za makampuni.
Sasa tukija kwetu Afrika, Tumezungukwa na rasilimali kibao lakini tunashindwaje kufika huko ?
mfano mdogo tu ukiunganisha Tanzania, Kenya, Uganda, Rwamda, Burundi, Sudan Kusini, Congo, Malawi, bado hupati bajeti ya trilioni 700
Mkuu 'Mkata uzi'
Mada kama hii inahitaji mjadala tulivu kabisa. Ni mada sahihi kabisa, pamoja na kwamba siyo muda sahihi kutokana na utawala uliopo ulioamua kujitwalia madaraka kwa nguvu.
Unaizungumzia Israel, ambayo ni taifa zima pamoja na udogo wake!
Fanya hivi: Elon Musk sasa hivi anazo bilion ngapi $825; pengine na zaidi; geuza hiyo iwe madafu.
Ni mwaka juzi (kama sikosei), mtawala wetu alitembelea UChina kwa ziara ya kikazi. Alikutana na Xi Jinping kama kawaida na picha tulionyeshwa. Tukaambiwa kwamba China inao uhitaji mkubwa sana wa Soya; tukiweza kulima soya ya kutosha zao letu halitakosa soko. Picha iliyoandamana na taarifa hizo ikiwaonyesha Mtawala wetu na Bwana Jinping ilionyesha kama Bwana Jinping anamsihi huyu mtawala wetu asiiachie fursa hiyo. Ni picha ambayo mwonekano wake ulinasa kabisa ndani ya akili yangu; na kila mara ninapoikumbuka inanisononesha sana.
Mtawala wetu alimaliza ziara yake na kurudi nyumbani, na hadi leo hii hajawahi tena kutamka chochote juu ya fursa ile iliyojadiliwa kule.
Sidhani kuwa anakumbuka chochote tena kuhusu ziara hiyo.
Kule kwa wajomba ambako wao wamejaliwa kuwa na utajiri unaotokana na mali asili ya gesi na mafuta, wao wameneemeka sana na raslimali yao hiyo.
Sijafuatilia kwa karibu zaidi walivyoweza kubana na kufanya mikataba iliyowanufaisha wao kiasi kile.
Nasi hapa tunazo raslimali kadhaa ikiwa ni pamoja na gesi kule Mtwara.
Wale wajomba wa Oman, na wao waliwagawia watu toka nje watumie raslimali yao ya gesi kama tunavyowapa sisi hao hao wenye utajiri mkubwa huko kwao?
Mikataba ya kuwagawia gesi waoman, kule Ntorya, Mtwara; kuna yeyote anayejuwa ni namna gani nasi itatuinua, kama ile ya kwao ilivyowainua wao?
Sasa leo hii hapa, mkuu wangu 'Mkata uzi', unazungumzia bajeti ya Israel, na kutufikiria nasi tuwe kama wao; angalao hata kwa robo tu, itawezekana kweli?
Ulishawahi sikia huko Israel wanafanya upuuzi kama unaofanyika hapa?
Hiyo bajeti ya Israel, unajuwa ni asili mia ngapi itatumika kiuhalisia na siyo kwa maigizo ya tarakimu kama ilivyo kawaida ya hii hapa kwetu? Sisi tunaweka manamba makubwa tu kama mapambo; kinachotekelezwa ni chini ya asili mia 30 ya kilichopangwa!
Nihitimishe kwa kusema kuwa pamoja na kuwa ni mada sahihi kabisa kujadiliwa, lakini nafikiri hukutumia mlinganisho sahihi. Umekwenda mbali mno na sisi tulipo. Jaribu kulinganisha vinavyokaribiana
Nakupongeza kwa mada sahihi, pamoja na hayo yote niliyoyagusia kuwa 'mismatch' na sisi.