Mkuu
ebaeban, wanaliongeleaje suala la Tanzania kuwahusisha FBI kupeleleza matukio madogo kabisa yanayotokea hapakwetu?
Kama sikosei Nyerere wanaemkubali ndio aliwanyima ubalozi wao hapa Tanzania na hadi leo hatuna ubalozi wa Israel kwetu, hilo hawakuliongelea? Binafsi, namkubali sana Mwl. Nyerere.
Kwa jina la mwenyezzi mungu; Poleni wote kwa janga na Msiba huu, Kwanza tendo hili HALIKUBALIKI kamwe na ni tendo la kikatiili kabisa. lina LAANIKA kwa wanaIMANI wa dini zote za mbinguni (ISLAM,CHRISTIAN,JUDISM) ... Hapa muhimu
Wandugu waislam hapa msichukulie kuwa FBI amekuja kuwatuhumu au kuwahusisha Muslims only, NO NO NO siyo hivyo.
hao FBI wanahakikisha kila uwezekano wa kumtambua aliye panga njama nzima na aliyetenda UHALIFU huo wa kulipua.
sasa wandugu kweli FBI hakaribishwi na wengi wetu kimaoni, Lakini je lingetupata msiiba huu kwetu kikweli, tungelikuwa na hali gani na hisia zepi juu ya Masuala ya upelelezi ? na Mengineyo? Wakati Serikali inajizoazoa nasi ni watu wakutosubiri tija rasmi. Tujifikirie na kuheshimu uchungu wa wenzetu.
Ukweli WaKRISTO hawa ni Jirani zetu, Wakabila wenzetu,ndugu zetu, Wananchi wenzetu upo uhusiano mkubwa ambao usioelezeka kimaandishi ni watu WAPOLE, WEMA na wenye UPENDO na kila mwanaAdamu hapa ulimwenguni, hiyo sifa inajulikana hata kwenye vitabu.
Kwa hiyo wamevumilia na kuikabidhi wakala husika kupeleleza na ni haki yao watakavyo, Nasi tuombe subira kidogo ili matokeo yafahamike. Mambo mengine yasiyotuhusu tafadhalini tusiya jali wala kushabikia. Janga hili ni usalama wa wote na nchi hi ni ya wote na kila mmoja ana uhuru wa kuamini vyake.
NINGEPENDA KUENDELEA lakini na wengine watoe maoni ya BUSARA na hekima.
Mungu Yaepushe mbali masaibu na balaa kwa Tanzania. amin