brasy coco
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 1,489
- 900
Kumbuka marekani kipindi hicho walitaka kuingia vitani upande wa ujerumani lakni pia kipindi hicho wayahudi wananguvu za kiuchumi na wapo balani ulaya na marekani na wamekamata sekta nyeti.walitumia ushawishi wao na kufaniwa kuishawishi marekani iingie vitani upande wa uingereza nao british wakaanza kuruhusu wale wazungu wayahudi waanze kurudi palestina.kidogokidogo wanarudi wananua ardhi toka kwa wapalestina.kumbuka hapa limebadilika jina tu watu ni walewale.
Baadae wayahudi wazungu wamekuwa wengi kutoka ujereman ,urusi na ulaya wakaanza kuwapiga vita wapalestina na kuteka ardhi .waingereza wakajitoa hapo .kuelekea na hadi mwaka 1948 wayahudi wazungu wakawa wamejitangazia taifa la israel wakipata full support toka nchi za ulaya na amerika.
Too cut the story short,Taifa la israel ndo likawepo hapo kwa kutumia nguvu za kivita.cha ajabu sasa waisrael eneo lote lilojulikana kama nchi ya yuda,na baadae samaria wayahudi wamewaachia wapalestina katika kile kilichoitwa unilateral disengagement miaka ya 90.katika maeneo yaliyoachwa ni kama bethelehem mji wa daudi.alipozaliwa yesu.
Wayahudi hawakupata kumkubali yesu na mpaka leo iko hivyo.hata wakristo walioka bethlehem ni wapalestina.
Wakristo waliopo israel ni arab israel siyo wayahudi.wayahudi wana dini yao inaitwa jew,dini ya kiyahudi na wanatumia Talmud na Torah na si bibilia.vitabu vyao vinamtaja yesu kama mtoto wa nje ya ndoa..etc.
ahsante