Netanyau huyu jamaa inawezekana ni muda mrefu alikuwa akitafuta sababu ya kuwachabanga Hamas. Hamas wakajichanganya. Wakajaa kwenye mfumo. Sasa kichaa kapewa panga. Anapasua roho zao.
Hamas wanasema wapo tayari kukabidhi nusu ya mateka. Neta anasema hata mkitaka kaeni nao sisi hatuna haraka nao. Na hata mkitukabidhi sisi tutaendelea kuwafirimba tu mpaka tuki come. Yaani wakijisikia kumaliza au kufika kileleni.
A new round of talks has taken place in Doha after Israel carried out airstrikes which killed hundreds.
www.bbc.com
Narudia tena japo watu huwa wananiponda na hii hoja.
Kwamba, baada ya Gaza kuendelea kustawi zaidi, Israle ikaona ikichelewa tu basi itakuja kuwa vigumu sana kuichukua Gaza.
Hivyo, Israel ikawatumia mapandikizi wake ndani ya Hamas kufanya mauji na utekaji ule ili kupata sababu. Kweli, wale mapandikizi waliwashawishi Hamas wengine wakajaa. Ikumbukwe, kuna tetesi kuwa, Israel ndiyo iliunda Hamas kuwapinga kina Yasser Arafat kutoka chama cha PLO ambacho ndiyo kilikuwa na nguvu na kuongoza Ukingo wa Magharibi. Inaonekana Hamas na Israel badae walitofautiana. Lakini tujiulize, kweli Israel hakuacha mapandikizi kwa tabia yake ikiwa inasemekana anaweka mapandikizi hadi Iran?
Ule mpaka waliopita Hamas Oktoba waliuchambua BBC siku moja, ulikuwa na ulinzi wa hali ya juu. Kwa mfano, kuna fensi imara na kuna wasichana ambao kazi yao ni kuangalia nyendo za Wapalestina upande wa pili bila kugeuka. Huwa wanapeana zamu. Ikitokea tatizo lolote wanapiga ving'ora. Mfano Wapalestina wengi kuusogelea mpaka. Jiulize, ilikuwaje Oktoba? Wale walinzi walienda wapi?
Ilikuwaje walinzi wanawaona Hamas wengi wanakuja na mapikipiki yao halafu hawatoi taarifa tu. Hivi kwa Israel alivyo, si angewasha chopa zake na kuwafagia Hamas wote kabla hawajavuka mpaka? Inasemekana, Egypt ilikuwa inajiandaa kuishambulia Israel miaka ya sitini lakini Israel ikawahi kuzishambulia chopa zote za Egypt. Ndiyo angeshindwa kwa Hamas waliokuwa wanakuja na mapikipiki! Lakini ilibidi iwe hivyo ili sababu ipatikane
Hivyo, kwa vyovyote vile, Israel alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kuichukua tena na kuimiliki moja kwa moja Gaza.
Ikumbukwe, Gaza ilishawahi kukaliwa na Israel na akaiachia miaka ya 2000 kwa makubaliano kwamba Egypt ataisimamia kitu kama hicho. Lakini sidhani kama Israel ana mpango wa kuiachia tena Gaza kwa sababu mbalimbali ikiwemo za kiuchumi.
Kwa dalili zilivyo. Wapalestina wataondoka Gaza. Rejea kauli za Trump kwamba anataka kuifanya Gaza kuwa sehemu ya utalii, na Wapalestina kuanza kupelekwa nchi nyingine. Kwa mfano USA amekubaliana na Libya kuwapokea Wapalestina milioni 1 kwa ahadi ya kupewa mamilioni ya dola.
Leo hii hata Hamas waseme wanaitambua Israel, bado hawatakaa Gaza. Gaza itachukuliwa na Israel kwa kigezo cha usalama lakini wana sababu zao.