Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Ijumaa iliyopita Marekani ilikuwa inaadhimisha kujiondoa rasmi nchini Afghanistan baada ya vita dhidi ya ulichokiita ugaidi vilivyochukua miaka 20.
Kuangukia mikononi mwa Taliban kwa mji wa Kabul kulitanguliwa na kuuliwa kwa askari 13 wa Marekani pamoja na 170 wa jeshi la Afghanistan mnamo Agosti 26.
Baada ya hapo kilichotokea kiliishangaza Marekani juu ya mafanikio ya vita dhidi ya ugaidi.
Baada ya tukio hilo la kushtusha raisi Biden alitoa tangazo la kujifariji kwamba walikuwa wametoa hukumu kwa Osama bin Laden na kwamba Alqaeda walikuwa wameshindwa.
Kwa hivyo ilikuwa ni wakati sahihi wa kumaliza vita hivyo.Lengo la kuifuta Alqaeda lilitakiwa liende sambamba na kusimamisha serikali ya kidemokrasia nchini Afghanistan kuchukua nafasi ya Taliban.
Jinsi vita hivyo vilivyoishia kulizusha mjadala iwapo vita dhidi ya ugaidi vinaweza kufanikiwa kweli kwa njia ya vita.
Kwa upande wa Israel tangu kuundwa kwake hapo mwaka 1948 ilianza na kupambana na makundi ya kutoka nchi za kiarabu yaliyojulikana kama Fedayeen.
Baadae ikafuatiwa na chama cha ukombozi cha Palestina cha PLO.
Pamoja na nguvu kubwa ambayo Israel imekuwa ikitumia lakini badala ya kuyamaliza makundi yanayopinga nayo kwa sasa ndio yameongezeka sana na kufikia karibu dazeni mbili yakitokea Gaza, Lebanon, Syria, Iraq, Yemen pamoja na ukingo wa magharibi.