Mwanajeshi wa kwanza wa Israel amethibitishwa kuuawa ndani ya Lebanon tangu uvamizi wa ardhini kuanza.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilitangaza katika taarifa kwamba Kapteni Eitan Yitzhak Oster, 22, aliuawa ndani ya Lebanon siku ya Jumatano.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa katika kitengo cha Egoz, cha makomandoo maalumu wa vita vya ardhini, IDF inasema.