Israel yathibitisha kumuua Mkuu wa Kijeshi wa Hamas mwezi Julai

Na ndio nimekuja kuielewa vizuri kipindi hiki kumbe kitabu chetu hakidanganyi alhamdulillah nimethibitisha hilo
 
Tangu nione ile video ya vijana wetu wakiuwawa kikatili kama vibaka sina sympathy na magaidi kabisa
 
Jeshi la Israel leo limethibisha kuuawa kwa mkuu wa jeshi la Hamas bwana Mohammed Deif kilichotokea 13 July 2024. Hamas wamekaa kimya kuhusu kifo cha huyu kamanda wao Mkuu.
Uongo hamas hajathibitisha wala hezbo awajasema kitu na wao huwa hawadanyi
 
wakiristo naona mkisikia kama hivi Roho nyeupe kwenu
Sie wakuvaa ngozi za mbuzi tukisikia upande wowote wa hizo dini za majahazi kimenuka sie kwetu furaha tu,,,apigwe mwarabu apigwe mzayuni kwetu sherehe tu.......tunasema malipo ni hapahapa duniani........mmoja anatuzingua na ugaidi mmoja analazimisha mambo ya upinde..........MIDdLeEAST BOMAYEEE
 
Muajemi kasrma haliwezi kupita hivi hivi.
Ngoja tuone
 
Kumbe una ndugu Palestine, Yemen,Iraq,Libya,Mali,Sudan na Afghanistan huku wewe ukiwa Kitunda Mwanagati mbona huendi kuwasaidia?
 
Kaka hii ni Aya ya ngapi na surat gani
 
Huyu yahaya Sinwar mbona wanamchelewesha kumpeleka kwa Allah
 
Hamas wamepata mapigo mazito mno, wamedhoofishwa tu ila kupotezwa kabisa sio rahisi.
 
Na sie tunaumia kwa kupotelewa na ndugu zetu wa Afrika huko Kenya ,Nigeria na Msumbiji hao akina boko haram sijui al shabab wakifanyaga yao mbona mnakenua tu
 

Chanzo cha picha,AFP
Jeshi la Israel linasema lilimuua mkuu wa jeshi la Hamas Mohammed Deif katika shambulio la anga huko Gaza tarehe 13 Julai.
Deif alilengwa katika shambulio la Israeli kwenye boma katika eneo la Khan Younis.
Jeshi la Israel wakati huo lilisema kuwa kamanda mwingine wa Hamas, Rafa'a Salemeh, aliuawa katika shambulio hilo , lakini lilisema halina uthibitisho wa mwisho juu ya hatima ya Deif.
Jeshi la Israel linasema kuwa limethibitisha kuwa mkuu wa jeshi la Hamas Mohammed Deif aliuawa katika shambulio la anga katika Ukanda wa Gaza mwezi uliopita.
Israel inasema Deif alikuwa mmoja wa watu waliohusika na kupanga mashambulizi ya Oktoba 7 kusini mwa Israel ambapo watu 1,200 waliuawa.
Tangazo la Israel linakuja siku moja baada ya kuuawa kwa kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismael Haniyeh, aliyeuawa mjini Tehran, na kamanda mkuu wa Hezbollah Fuad Shukr, ambaye aliuawa katika shambulio la anga la Israel katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Taarifa kutoka kwa jeshi la Israel ilisema kuwa "kufuatia tathmini ya kijasusi, inaweza kuthibitishwa kuwa Mohammed Deif aliuawa" katika shambulio la Julai 13.
Mamlaka ya afya ya Gaza inayosimamiwa na Hamas ilisema wakati huo kwamba mashambulizi ya anga yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 90, lakini ikakana kuwa Deif alikuwa miongoni mwa waliofariki.
Mohammed Deif alikuwa mkuu wa Brigedi ya Izzedine al-Qassam, kitengo cha kijeshi cha kundi la Hamas.
Alifungwa gerezani na mamlaka za Israel mwaka 1989, ambapo baada ya hapo alianzisha Brigedi hiyo kwa lengo la kuwakamata wanajeshi wa Israel.
Israel ilimshutumu kwa kupanga na kusimamia mashambulizi ya mabasi yaliyoua makumi ya Waisraeli mwaka 1996, na kuhusika katika kuwakamata na kuwaua wanajeshi watatu wa Israel katikati ya miaka ya 1990.
Anajulikana pia kusaidia katika kufanikisha ujenzi wa mahandaki ambayo yamewaruhusu wapiganaji wa Hamas kuingia ndani ya Israeli kutoka Gaza.
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah
BBC
 
Na sie tunaumia kwa kupotelewa na ndugu zetu wa Afrika huko Kenya ,Nigeria na Msumbiji hao akina boko haram sijui al shabab wakifanyaga yao mbona mnakenua tu
Basi wewe endelea kuumia na kusapoti kwa wanaouana kwa ujahili, sisi tunaendelea kusimama na freedom fighters
 
Unafa masihara na MUNGU wa israel

Kabla hamjaanza kushabikia vita someni biblia ayaaa
Si wenzenu tunawaombea tu Amani basi

Ila atakayeumia zaidi tunamjua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…