Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Waziri wa ulinzi wa Israel amesema nchi yake iko vitani maeneo saba tofauti.Akaongeza kusema kuwa kutokana na hilo tayari wameshaanza kushambulia kwa nguvu maeneo sita kati ya hayo kulipiza kisasi.
Maeneo hayo aliyataja kuwa ni Iraq,Syria,Lebanon na Yemen.Mengine ni Gaza,ukiongo wa Magharibi na Iran.
Kwa upande wa wapiganaji wa Houth wa Yemen wamekuwa na hamasa za kupigana siku baada ya siku na kutokutishwa na muungano unaoongozwa na Marekani wenye nia ya kuwanyamazisha.
Hapo jana wanamgambo hao kutoka nchi maskini walifanikiwa kuipiga meli ya United VIII inayomilikiwa na shirika la MSC Mediterranean Shipping lenye uhusiano na Israel.Meli hiyo ilikuwa ikitokea Saudi Arabia kuelekea Pakistan.
Mbali na shambulio hilo la meli kiongozi wa kijeshi ya Yemen,Yahya Saree amesema vikosi vyake vilishambulia mji wa bandari wa Israel wa Eliat.Israel imekiri kupambana na makombora hayo kutoka Yemen bila kuweka wazi iwapo kulikuwa na hasara yoyote iliyosababishwa nayo.
Muungano wa kulinda bahari ya Red Sea umesema siku ya jana kudondosha droni 12,makombora 3 ya kupiga meli na makombora 2 ya kupiga mbali ambayo huenda yalikuwa yakielekea Israel.