Israel yaufyata mkia

Israel yaufyata mkia

Ngoja zamu ya Hamas iishe, then itafata ya Jordan...!

Narudia tena ulichoandika kwa lugha rahisi...! Kwamba

"Kwa sasa hatutaki maneno na Herzibula, ila kama watatulazimisha... Basi JORDAN italipa gharama kubwa...!"

wanachomaanisha ni kwamba wao hawatachagua pa kupiga, wao wataipiga Jordan, ambcho hawatataka tu ni yale maneno ya kusema kwa nini apige Uwanja wa shule, kwa nini apige Ukumbi wa Disco, vinahusiana nini na Herzibulah....!

Hicho ndo hawatataka kusikia.
Kafiri ashajijua akifa motoni tu kwa hivyo anaweza kufanya anachoweza
 
Rais Isaac Herzog wa Israel amedai kuwa, utawala huo wa Kizayuni hauna azma ya kuingia vitani na Harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon katika upande wa kaskazini, siku chache baada ya viongozi wa Marekani kuwatahadharisha watawala wa Israel kuhusu ugumu na hatari ya kuendesha vita viwili kwa wakati mmoja; upande wa kusini na Harakati ya Hamas ya Palestina na upande wa kaskazini na harakati yenye nguvu kubwa ya kijeshi, Hizbullah.

Herzog alisema hayo jana katika kikao na waandishi wa habari akiwa pamoja na mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kueleza kuwa: Hatutaki makabiliano katika mipaka ya kaskazini, lakini iwapo Hizbullah itatuburuza kwenye vita, Lebanon italipa gharama kubwa.

Kauli ya Herzog imekuja chini ya wiki moja baada ya Rais Joe Biden wa Marekani na washauri wake wakuu kuwaonya viongozi wa utawala ghasibu wa Israel wasijaribu kuingia katika vita na migogoro na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah.

Aidha hivi karibuni, Hizbullah ya Lebanon ilitangaza kuwa imetoa kipigo kikali katika mashambulio iliyofanya dhidi ya ngombe za jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mashamba ya Shabaa ya ardhi ya Lebanon inayokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Hii ni katika hali ambayo, jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limekiri kwamba, askari zaidi ya 300 wa utawala huo wameuawa tangu kuanza kwa vita vya Kimbunga cha al-Aqsa mnamo Oktoba 7.

Operesheni hiyo hadi sasa imepelekea kuangamizwa Wazayuni wasiopungua 1,500 na kujeruhiwa karibu wengine 5,000. Pia, Wazayuni wengine wapatao 200 wamekamatwa mateka na wapigania uhuru wa Palestina.
Rubbish
 
Back
Top Bottom