Issa Michuzi na vekesheni

Status
Not open for further replies.
Hapa naona kuna double standards. Juzi iliwekwa thread ya kumshangaa JK kukutana na mcheza filamu Steven Seagal, na watu waliona kama ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Leo hii UM analeta thread ya mmoja ya watu walioongozana na JK huko huko Marekani kupiga picha na kuweka katika blogu yake, lakini miongoni mwa hao waliomshangaa JK wanamtetea mtu aliyeongozana naye kufanya kazi binafsi, na kudai si matumizi mabaya ya fedha na muda, ila ni wivu!! Basi kumbe hata JK tusimuonee wivu, tuache akutane na wacheza filamu wengi zaidi. Kwa anayetaka kujua ile thread, iko HAPA
 


Mkuu unanikumbusha yule Pundit....sijui yuko wapi yule...ama?
 
Mkuu unanikumbusha yule Pundit....sijui yuko wapi yule...ama?

Pundit haishi kuwa quote Freud, Shakespeare na Jay-Z.Anaingiaingia humu mara chache chache, nafikiri kazi zimemtinga.

He surely would have lamented the remarkable macabre folly of indefatigably defending the indefensible.
 
Last edited:
Mkuu acha wivu wa kike!
 

Lakini Uwiano, hivi hawa wanaanchi wa JF si ndio select group walio na mwamko, au niseme uelewa wa juu zaidi na misimamo ya kuchukia ufisadi? Iweje sasa hawaoni tatizo hapa? Ni hawajali au hawaelewi, au unafiki au?
 
Lakini Uwiano, hivi hawa wanaanchi wa JF si ndio select group walio na mwamko, au niseme uelewa wa juu zaidi na misimamo ya kuchukia ufisadi? Iweje sasa hawaoni tatizo hapa? Ni hawajali au hawaelewi, au unafiki au?

Nadhani unafiki, haupendwi ukweli bali ushabiki.

Hili tatizo ndugu yangu Dilunga, na safari zisizo na kichwa wala miguu, kwa watumishi wa umma hapa Tz ni kubwa kuliko linavyoonekana. Bahati nzuri kwa Michuzi imekuwa freudian slip, lakini bado watu wameghubikwa na kasumba za kuonea wivu, ale sehemu yake etc.

Namna hii hatufiki huko tunakotegemea kufika especially kuhusiana na ufisadi.
 
hivi wewe ulitaka michuzi afanyaje/aandikeje/aweke picha zipi kwenye blog yake?
 
Mkuu acha wivu wa kike!

Stop the ignorant chauvinism.Hunijui sikujiu utasemaje nina wivu kwa clown kitoko kama Michuzi? Anakokuja kutembea kwa kudra za Kikwete na misuse of public funds sisi wengine ni stomping grounds tu, tena bila kutumia hela ya mtu.Una fly in Friday night out Sunday evening, vacation weekend yoyote tu.

Una ji expose tu kwamba na wewe uko kwenye caliber hiyo hiyo ndiyo maana you can't tell the difference.
 
nadhani hata hao wanafadhili blog la michuzi inabidi wafikire marambili.hili blog halina manufaa yoyote zaidi ya ujinga.hiz ni zama za kuandika mambo yenye manufaa kwa taifa na wadau wake (yaani walipa kodi)siyo picha zisizokuwa na maana.kila mtu akisema aweke picha za anachofanya ulaya au Marekani haisaidi.Nahuyo anayee sema Michuzi ni rafiki wa Wawatanzania wote wanish ughaibuni anakosea.Mimi naishi ughaibuni na sio rafiki wa michuzi, labda tuu akianza kuandika mambo ya kujenga taifa yenyekueleweka.
wenu,
Susu,
London-UK
 

Huo mfano umenichekesha, ''truck driver'' ishu si safari ishu siyo yatokanayo na safari ''truck driver'' sanasana atanunua mkaa highway basi, teh teh teh
lakini nakubali you can't trade your Phd for safari za nje, unless you are uncertain of what your Phd worth.
 
Hakika hakuna mtu mshamba kama wewe kumshambulia mtu ambaye kosa lake kwa upande wako ni kusafiri.

Michuzi kwa taarifa yako hajaanza leo kusafiri na hiyo kusema 'vekesheni' ni staili yake ya kusema yuko safari. Ati una phd na husafiri, hahahaahaaa!

Halafu ni aibu kwa jf kushabikia hoja za kipuuzia kama hizi. Kama mna mpango wa kumhujumu michuzi semeni ijulikane maana si la kuficha kwamba jamaa kawazidi kete kwa ubunifu. Sio copy and paste za habari za watu. Naona hata video mmeamia kumuiga hahahaa jf mnachemsha. Ndio maana hata kwenye matangazo kawapiga bao.

Halafu wewe mshamba wa vekesheni za michuzi umekera umma kama nini sijui, angalia jinsi ulivyokosa sapoti, na wewe umeonekana mpumbavu. Unaelewa michuzi ana uwezo wa kusafiri popote duniani kwa pesa yake (ya blogu tu, angalia matangazo bwelele) na wewe na phd yako feki ya kuliliasafari utakalagha baho.

Tarishi



 

Tarishi studying in Ukraine..lol What exactly r u studying in there? stupidity?
 
Mwacheni nanihii naye afaidi japo kidogo keki ya taifa, mbona Vasco da Gama ye hamumsemi! kwani anatumia pesa ya nani? nanihii ametumwa na sirikali anafanya alichotumwa na baada ya kazi ni bata tu! we unafikiri kule Hollyhood alifikaje kama sio Da Gama ndio alienda nae, sa umeshajiuliza Da Gama alienda huko kufanya nini? na kwa faida ya nani?
 
Tarishi nakwambia na ninakusisitizia Michuzi ni mtu mdogo sana hapa JF na Michuzi hawezi shindana na hii JF na analijua yeye ni mtu mdogo sana kwa hiyo JF haina mpango wa kumhujumu misupu.
 
Uwiano usishangae sana
Hakuna kesi isiyo na mtetezi walah.
Umeuliza swali makini sana na naona majibu yanakuja kiutumbo utumbo hapa.

Mimi ninavyoona ni kwamba upo sahihi unaposema kwa nini atumie hela za walipa kodi kwa kufanya kazi binafsi wakati yupo vekesheni. Ni kwamba huu ni udhaifu mkubwa ktk kusimamia hela za serikali kwa maofisa wanaokiuka maadili ya kazi zao.

Na mdau mmoja amejibu hapa kwamba vekesheni ni lugha ya kisanii inayoutmika ktk blog ya michuzi. Mie napinga hilo kwani michuzi hakuwahi kufafanua kuwa anaposafiri nje kikazi ni vekesheni.

Jamani tuwe na nadhamu na pesa ya umma kwani kuna watoto wanafariki hata kabla´na baada ya muda mfupi wa kuzaliwa kwa ukosefu wa fedha za kununulia huduma za kuwakinga na kuwalinda. Kuweni na huruma maafisa wa umma mnaotapanya kodi zetu ovyo.
 
Unayo takwimu kuonesha umma ulivyokosewa na mleta hoja???
(nshaaza kuwa uwiano sasa lol)

Ila ujue humu hoja hujobiwa kwa hoja na si matusi mkuu. Michuzi ni rafiki yangu sana ila siwezi kumchekea endapo atafanya ukiukaji wowote kwani najua hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya. Kila jambo limekusudiwa na limepagwa.
 

Waambie hawa wapuuzi, wamekosa ya kujadili humu. Kama hamjui fani zinaendeshwaje, mkae kimya sio kuropoka tu. Huyu ni msanii wa fani ya blog, na anatumia lugha mbalimbali kunakshi blog yake, kwani mtu akienda kwenye msafara wa rais ndo hatakiwi kujipumzisha? hata mlinzi wa rais anapata time ya kupumzika na kujivinjari, acheni roho za korosho. Bro kamua mtu wangu, kula bata!
 
Ndoano moja huvua samaki wengi na tofauti ila chambo huwa si kile kile
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…