Issa Michuzi na vekesheni

Issa Michuzi na vekesheni

Status
Not open for further replies.
Hapa naona kuna double standards. Juzi iliwekwa thread ya kumshangaa JK kukutana na mcheza filamu Steven Seagal, na watu waliona kama ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Leo hii UM analeta thread ya mmoja ya watu walioongozana na JK huko huko Marekani kupiga picha na kuweka katika blogu yake, lakini miongoni mwa hao waliomshangaa JK wanamtetea mtu aliyeongozana naye kufanya kazi binafsi, na kudai si matumizi mabaya ya fedha na muda, ila ni wivu!! Basi kumbe hata JK tusimuonee wivu, tuache akutane na wacheza filamu wengi zaidi. Kwa anayetaka kujua ile thread, iko HAPA
 
Uwiano Maalum,

This is the classic "Freudian Slip". Most of us know that Michuzi is a sorry excuse for a clown, lakini this time katika ku clown huku na kuita safari ya nje iliyo katika vocation yake kuwa ni vacation, ame expose ukweli kwamba huko wanakoenda hamna wanachofanya zaidi ya vacation.

I would love this to be a case of a succintly eloquent "Shakespearean Fool" exposing the illdoings of the ruling class in a tragicomic way, but the reality is Michuzi can hardly be said to posses such sophistication.Sometimes the truth cannot be bottled and pressures simpletons such as Michuzi into "Freudian Slips" such as this.

Trouble is, this "dramatic irony', indeed a gem, is wasted on a lot of us.

Bigger trouble is, if the president is surrounded by clowns like these it sort of give you an idea of how much of a clown this very same president must be.


Mkuu unanikumbusha yule Pundit....sijui yuko wapi yule...ama?
 
Mkuu unanikumbusha yule Pundit....sijui yuko wapi yule...ama?

Pundit haishi kuwa quote Freud, Shakespeare na Jay-Z.Anaingiaingia humu mara chache chache, nafikiri kazi zimemtinga.

He surely would have lamented the remarkable macabre folly of indefatigably defending the indefensible.
 
Last edited:
Naelewa vizuri maudhui ya blog ya Michuzi, kuna mtu alieleza kuwa dissapointed na Clouds FM kuhusu kuiita Oval Office "Overhaul Office" mimi nikawa wa kwanza kusema kwamba kutegemea seriousness kutoka Clouds FM ni sawa na kutegemea seriousness kutoka kwa Michuzi, kwa hiyo mimi naelewa maudhui ya blog ya Michuzi, ndiyo maana nikamwita clown.

Kisichoeleweka na wengi ni kwamba katika kujitia u clown Michuzi (which is just a mask for his ignorance, Mzee Jongo style) Michuzi safari hii kasema ukweli bila kukusudia, kwa hiyo Freudian slip ya kusema anaenda vacation, ni kweli rais Kikwete akienda nje largely anaenda vacation, lakini ukweli huu unakuwa choreographed na PR nyingi aonekane anafanya kazi, sasa safari hii mpiga picha wake mwenyewe kateleza ulimi na kureveal kwamba huko hamna chochote zaidi ya vacation, which is the truth.

Unaweza kuniambia Kikwete kafanya kitu gani huko cha maana? Kukutana na hao ma doctors na kijiaward chao mshenzi? Umesoma article ya NYT kuhusu afya za kinamama wanaojifungua katika hali mbaya Tanzania?

Ona hapa

https://www.jamiiforums.com/habari-...-tanzania-where-life-s-start-deadly-risk.html

Rais wa nchi kama hii anastahili award? Kitu gani, kukutana na Obama na kuendeleza uomba omba?

Pleeease!

Wanaenda vacation tu, na big mouth Michuzi ka expose hilo kwa wale wagumu wa kuelewa, sijui mnataka sign kutoka mbinguni ndiyo muelewe, na naona hata hiyo mta i doubt.
Mkuu acha wivu wa kike!
 
Kama mambo kama haya yanashindwa kuonekana, bado tunasafari ndefu kuelekea accountability, responsibility na rule of law. Hakuna mwenye uchungu na pesa za walipa kodi, hakuna mwenye kuhoji pesa hizi zinatumika vipi na kwa nini. Kuna kukesha kutafuta mchawi wakati kinachotula ki kwenye nguo.

... misuse of resiurces kweye government institutions, huko ndio ufisadi ulipojichimbia na kujikita mizizi.

Kama hakuna anayeona kuna tatizo kwenye hili suala la Michuzi kutumia muda wa mwajiri, ambao kwa muda huo ndipo anapolipwa na fedha za walipa kodi; kufanya mambo binafsi...

Lakini Uwiano, hivi hawa wanaanchi wa JF si ndio select group walio na mwamko, au niseme uelewa wa juu zaidi na misimamo ya kuchukia ufisadi? Iweje sasa hawaoni tatizo hapa? Ni hawajali au hawaelewi, au unafiki au?
 
Lakini Uwiano, hivi hawa wanaanchi wa JF si ndio select group walio na mwamko, au niseme uelewa wa juu zaidi na misimamo ya kuchukia ufisadi? Iweje sasa hawaoni tatizo hapa? Ni hawajali au hawaelewi, au unafiki au?

Nadhani unafiki, haupendwi ukweli bali ushabiki.

Hili tatizo ndugu yangu Dilunga, na safari zisizo na kichwa wala miguu, kwa watumishi wa umma hapa Tz ni kubwa kuliko linavyoonekana. Bahati nzuri kwa Michuzi imekuwa freudian slip, lakini bado watu wameghubikwa na kasumba za kuonea wivu, ale sehemu yake etc.

Namna hii hatufiki huko tunakotegemea kufika especially kuhusiana na ufisadi.
 
Nadhani unafiki, haupendwi ukweli bali ushabiki.

Hili tatizo ndugu yangu Dilunga, na safari zisizo na kichwa wala miguu, kwa watumishi wa umma hapa Tz ni kubwa kuliko linavyoonekana. Bahati nzuri kwa Michuzi imekuwa freudian slip, lakini bado watu wameghubikwa na kasumba za kuonea wivu, ale sehemu yake etc.

Namna hii hatufiki huko tunakotegemea kufika especially kuhusiana na ufisadi.
hivi wewe ulitaka michuzi afanyaje/aandikeje/aweke picha zipi kwenye blog yake?
 
Mkuu acha wivu wa kike!

Stop the ignorant chauvinism.Hunijui sikujiu utasemaje nina wivu kwa clown kitoko kama Michuzi? Anakokuja kutembea kwa kudra za Kikwete na misuse of public funds sisi wengine ni stomping grounds tu, tena bila kutumia hela ya mtu.Una fly in Friday night out Sunday evening, vacation weekend yoyote tu.

Una ji expose tu kwamba na wewe uko kwenye caliber hiyo hiyo ndiyo maana you can't tell the difference.
 
nadhani hata hao wanafadhili blog la michuzi inabidi wafikire marambili.hili blog halina manufaa yoyote zaidi ya ujinga.hiz ni zama za kuandika mambo yenye manufaa kwa taifa na wadau wake (yaani walipa kodi)siyo picha zisizokuwa na maana.kila mtu akisema aweke picha za anachofanya ulaya au Marekani haisaidi.Nahuyo anayee sema Michuzi ni rafiki wa Wawatanzania wote wanish ughaibuni anakosea.Mimi naishi ughaibuni na sio rafiki wa michuzi, labda tuu akianza kuandika mambo ya kujenga taifa yenyekueleweka.
wenu,
Susu,
London-UK
 
Mkuu... MBona unajiaibisha??? Do you think ni safari tu ndio kitu kizuri?? can you trade your PhD kwa ajili ya safari za nje?

Kila mmoja ana nafasi yake na kuna mambo unapata ambayo michuzi hatakaa apate, kila mtu na nafasi yake

Vipi kuhusu truck drivers? they travel alot... do you like to be one?

Huo mfano umenichekesha, ''truck driver'' ishu si safari ishu siyo yatokanayo na safari ''truck driver'' sanasana atanunua mkaa highway basi, teh teh teh
lakini nakubali you can't trade your Phd for safari za nje, unless you are uncertain of what your Phd worth.
 
Hakika hakuna mtu mshamba kama wewe kumshambulia mtu ambaye kosa lake kwa upande wako ni kusafiri.

Michuzi kwa taarifa yako hajaanza leo kusafiri na hiyo kusema 'vekesheni' ni staili yake ya kusema yuko safari. Ati una phd na husafiri, hahahaahaaa!

Halafu ni aibu kwa jf kushabikia hoja za kipuuzia kama hizi. Kama mna mpango wa kumhujumu michuzi semeni ijulikane maana si la kuficha kwamba jamaa kawazidi kete kwa ubunifu. Sio copy and paste za habari za watu. Naona hata video mmeamia kumuiga hahahaa jf mnachemsha. Ndio maana hata kwenye matangazo kawapiga bao.

Halafu wewe mshamba wa vekesheni za michuzi umekera umma kama nini sijui, angalia jinsi ulivyokosa sapoti, na wewe umeonekana mpumbavu. Unaelewa michuzi ana uwezo wa kusafiri popote duniani kwa pesa yake (ya blogu tu, angalia matangazo bwelele) na wewe na phd yako feki ya kuliliasafari utakalagha baho.

Tarishi



issa michuzi kaandika kwenye blog yake kuwa yuko vekesheni, na kweli anatundika picha mbalimbali akiwa anajivinjari sehemu mbalimbali nchini marekani.

View attachment 4638

ninachojiuliza, je ni kweli amejilipia vekesheni hiyo yeye mwenyewe au yuko kwenye msafara wa rais kikwete nchini marekani?

View attachment 4639

kama yuko kwenye msafara wa rais, ina maana analipiwa gharama zote na pesa ya walipa kodi. Je ni halali kufanya ziara ya kikazi kuwa vekesheni yake na kufanya shughuli binafsi kama alivyoonyesha kwenye picha mbalimbali kwenye blog yake?


View attachment 4640

kwa mshahara wa mfanyakazi wa serikali kama issa, sio rahisi kufanya vekesheni sehemu mbalimbali za dunia, na kujigharimia mwenyewe. Je issa michuzi anapata wapi pesa hizi?

Je, issa michuzi ni fisadi au anafadhiliwa na mafisadi kwenye safari zake? Kama mfanyakazi wa serikali, issa michuzi anatumia muda kiasi gani ofisini, akilitumikia taifa kama muda mwingi anakuwa safarini, na kwa nini anatumia muda wake mwingi kwenye shughuli zake binafsi kama safari zake zinalipiwa na walipa kodi?

Naomba kueleweshwa na yeyote mwenye kujua zaidi.

Picha zote zimetoka michuzi blog.
 
Hakika hakuna mtu mshamba kama wewe kumshambulia mtu ambaye kosa lake kwa upande wako ni kusafiri.

Michuzi kwa taarifa yako hajaanza leo kusafiri na hiyo kusema 'vekesheni' ni staili yake ya kusema yuko safari. Ati una phd na husafiri, hahahaahaaa!

Halafu ni aibu kwa jf kushabikia hoja za kipuuzia kama hizi. Kama mna mpango wa kumhujumu michuzi semeni ijulikane maana si la kuficha kwamba jamaa kawazidi kete kwa ubunifu. Sio copy and paste za habari za watu. Naona hata video mmeamia kumuiga hahahaa jf mnachemsha. Ndio maana hata kwenye matangazo kawapiga bao.

Halafu wewe mshamba wa vekesheni za michuzi umekera umma kama nini sijui, angalia jinsi ulivyokosa sapoti, na wewe umeonekana mpumbavu. Unaelewa michuzi ana uwezo wa kusafiri popote duniani kwa pesa yake (ya blogu tu, angalia matangazo bwelele) na wewe na phd yako feki ya kuliliasafari utakalagha baho.

Tarishi

Tarishi studying in Ukraine..lol What exactly r u studying in there? stupidity?
 
Mwacheni nanihii naye afaidi japo kidogo keki ya taifa, mbona Vasco da Gama ye hamumsemi! kwani anatumia pesa ya nani? nanihii ametumwa na sirikali anafanya alichotumwa na baada ya kazi ni bata tu! we unafikiri kule Hollyhood alifikaje kama sio Da Gama ndio alienda nae, sa umeshajiuliza Da Gama alienda huko kufanya nini? na kwa faida ya nani?
 
Tarishi nakwambia na ninakusisitizia Michuzi ni mtu mdogo sana hapa JF na Michuzi hawezi shindana na hii JF na analijua yeye ni mtu mdogo sana kwa hiyo JF haina mpango wa kumhujumu misupu.
 
Uwiano usishangae sana
Hakuna kesi isiyo na mtetezi walah.
Umeuliza swali makini sana na naona majibu yanakuja kiutumbo utumbo hapa.

Mimi ninavyoona ni kwamba upo sahihi unaposema kwa nini atumie hela za walipa kodi kwa kufanya kazi binafsi wakati yupo vekesheni. Ni kwamba huu ni udhaifu mkubwa ktk kusimamia hela za serikali kwa maofisa wanaokiuka maadili ya kazi zao.

Na mdau mmoja amejibu hapa kwamba vekesheni ni lugha ya kisanii inayoutmika ktk blog ya michuzi. Mie napinga hilo kwani michuzi hakuwahi kufafanua kuwa anaposafiri nje kikazi ni vekesheni.

Jamani tuwe na nadhamu na pesa ya umma kwani kuna watoto wanafariki hata kabla´na baada ya muda mfupi wa kuzaliwa kwa ukosefu wa fedha za kununulia huduma za kuwakinga na kuwalinda. Kuweni na huruma maafisa wa umma mnaotapanya kodi zetu ovyo.
 
Hakika hakuna mtu mshamba kama wewe kumshambulia mtu ambaye kosa lake kwa upande wako ni kusafiri....Halafu wewe mshamba wa vekesheni za michuzi umekera umma kama nini sijui, angalia jinsi ulivyokosa sapoti, na wewe umeonekana mpumbavu. Unaelewa michuzi ana uwezo wa kusafiri popote duniani kwa pesa yake (ya blogu tu, angalia matangazo bwelele) na wewe na phd yako feki ya kuliliasafari utakalagha baho.

Tarishi
Unayo takwimu kuonesha umma ulivyokosewa na mleta hoja???
(nshaaza kuwa uwiano sasa lol)

Ila ujue humu hoja hujobiwa kwa hoja na si matusi mkuu. Michuzi ni rafiki yangu sana ila siwezi kumchekea endapo atafanya ukiukaji wowote kwani najua hakuna kitu kinachoitwa bahati mbaya. Kila jambo limekusudiwa na limepagwa.
 
Sasa mnataka kuchemka, kama mmekosa thread za kuanzisha bora mtafute wimbo mmoja hapa tuujadili.
Hiyo lugha ya vekesheni ni humour anayoitumia michuzi kama msanii katika fani ya ku-blog. Kama unashangaa kutumia vekesheni mbona huulizi kwanini anajiita ''nanihii'', au unadhani ana jina?

Waambie hawa wapuuzi, wamekosa ya kujadili humu. Kama hamjui fani zinaendeshwaje, mkae kimya sio kuropoka tu. Huyu ni msanii wa fani ya blog, na anatumia lugha mbalimbali kunakshi blog yake, kwani mtu akienda kwenye msafara wa rais ndo hatakiwi kujipumzisha? hata mlinzi wa rais anapata time ya kupumzika na kujivinjari, acheni roho za korosho. Bro kamua mtu wangu, kula bata!
 
Waambie hawa wapuuzi, wamekosa ya kujadili humu. Kama hamjui fani zinaendeshwaje, mkae kimya sio kuropoka tu. Huyu ni msanii wa fani ya blog, na anatumia lugha mbalimbali kunakshi blog yake, kwani mtu akienda kwenye msafara wa rais ndo hatakiwi kujipumzisha? hata mlinzi wa rais anapata time ya kupumzika na kujivinjari, acheni roho za korosho. Bro kamua mtu wangu, kula bata!
Ndoano moja huvua samaki wengi na tofauti ila chambo huwa si kile kile
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom