Tuwasilishe kwa mwajiri wake? Wafanyakazi wa serikali wangapi wanachambuliwa hapa kwa kufanya yasiyoridhisha na hatusemi "mtafute mwajiri wake"? Hiyo standard imeanza lini hapa?
Mwawado, brother/sister, unakosea ndugu yangu. Umuhimu wa kutupa habari haumaanishi apate leseni ya kuwa kafisadi fulani ka kuchanganya mambo binafsi na kazi za umma, tena za msafara wa Rais.
Hizo habari tumeshamlipa akatupe kupitia DAILY NEWS, la sivyo astaafu afanye bloging full time aendelee na safari za "vekesheni" kwa hela yake.
Katika maswala ya maadili ya kazi, kuna kitu kinaitwa muonekano wa mabaya, appearance of impropriety. Iwapo kazi yako wewe ni kupiga picha za DAILY NEWS, halafu tunakuona picha hizo hizo zinatokea DAILY NEWS na MICHUZI au nusu zinatokea DAILY NEWS, na nusu zinatokea MICHUZI, ni lazima tutajiuliza, je ulizipiga katika muda gani, wa kazi wa kwako? Na zile zilizotokea kote kote (video za MBAGALA, picha za JK ziarani, mahojiano na DEWJI) umezipiga katika muda wako, au? Nani ana miliki hizi picha, serikali au wewe?
Angalia unavyo ishusha forum ambayo na wewe ni mshiriki just kumpamba MICHUZI ambae unamwona ni deified.
Look here, Mkuu Mwawado. Michuzi sio untouchable. Hivi unavyoona hapa watu 90 wamemsapoti kumi wameona kuna tatizo basi ni hivyo hivyo hata huko serikalini pia. Kuna mkulu mmoja huko serikali ameona MICHUZI yuko kwenye msafara akaenda kupiga picha na li dildo, na hakupenda. Na huyo bosi wa Michuzi nae sio untouchable. Na yeye (bosi wake) hapendi watu wamshangae kwamba anatuma mwandishi kwenye msafara wa Rais mtu asiye na maadili ya kazi wala ya kijamii. Yana mwisho...