sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,687
- 1,111
Ni mshtuko mkubwa kwa Taifa baada ya Rais mteule SSH kutoa taarifa juu ya fedha za operation plea bargain kutojulikana ziliwekwa kwenye akaunti gani.
Urais ni taasisi,aliyeitumia sheria kuamuru itumike hayupo duniani,wasaidizi wake ndani ya taasisi ya urais wapo, maanake tuipe muda tume ilyoteuliwa kushughulikia haya mambo ili tusije tukafanya makosa ya kiufundi.
Tanzania inafuata mfumo wa jumuiya ya madola,katika moja ya hotuba zake mh. Rais aliwahi kusema msiwakate watu kama uchunguzi haujakamilika,Waingereza wanatumia sana mfumo,kwa kuogopa kuingiza serikali kwenye mgogoro usio na tija na kulipa fidia kubwa kuwasafisha.
Wahenga wanasema kila kitabu na zama zake,Rais Samia alikuwa makamu wa mtangulizi wake,lakini tabia na mienendo ya mtangulizi wake huenda ilimuweka kando katika baadhi ya maamuzi hasa binafsi,angekuwa hana nia njema huenda yangepita,kama Jk alivyozoea kusema ni upepo tu huo utapita.
Hoja yangu ni juu ya waathirika wa operation saka fedha kwa njia haramu ambayo ilikuwa na baraka za ikulu,nini nafasi yao kutokana na sakata hili!
Nashauri kamati hiyo iwarudie watuhumiwa hao ambao ndiyo walikuwa vyanzo vya makusanyo hayo yasiyojulikana ni kiasi gani,na huko China zimewekwa kwenye akaunti ipi.
Nafasi ya kuwarudia wahanga hawa ni kubwa sana kupata ukweli wa sakata lenyewe japo wengine walikwisha kufa huenda kwa mshtuko wa dhuluma hii,ikithibitika kuna uonevu wafidiwe na wasafishwe kwa jamii.
Rais apewe ushiriano na kamati aliyo iunda ili zoezi lisilete athari kwa Taifa. Na kwa kuwa tuna mashirikiano mazuri na China kazi haitakuwa ngumu.
Wapo wahusika wakuu, hawa hawahitaji uchunguzi kuwakamata,aliyekuwa DPP Biswalo atiwe nguvuni atueleze fedha zilielekezwa wapi, na maadili ya utumishi wa umma yanamtaka afanye nini inapotokea saga kama hilo.
Mwisho, tumpe Rais na kamati yake muda ili ufanisi uwe mkubwa,tumshauri kwa njia ya kuisadia nchi na siyo kuharibu ushahidi.