IST ina tatizo la coolant kutorudi kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank

IST ina tatizo la coolant kutorudi kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank

Thermostat ndiyo zinatolewa kwa sababu mazingira yetu (Tanzani & Africa generally) ni ya joto. Miji mingi ya Japan ina freeze, mf. Nagoya wanakotengeneza hizi gari hali yake ni baridi muda mwingi (10°,11°,12° etc) ndo maana wanaweka thermostat. Changamoto hiki kifaa kinaweza kumisbehave kikaziba na kuzuia Coolant isiende kwenye engine na mpaka ujue tayari ushakaanga cylinder head. Bora kuitoa ili uwe safe zaidi
 
Habari Wakuu!

Naomba msaada wa kiufundi kwa IST kutorejesha coolant kwenye rejeta kutoka kwenye reserve tank ambayo imekuwa ikimwagika baada ya kujaa. Nimejaribu kubadilisha kifuniko cha rejeta lakini tatizo bado linaendelea.
Hujafanya coolant bleeding yaani kuondoa hewa kwenye mzungyko wa coolant. Compression au circulation ya coolant inakuwa ndogo sababu kuna hewa kwenye coolant system na hamna pressure ya kutosha. Hii itasababisha engine ku overheat Weka coolant kwenye radiator halafu bonyeza coolant pipes zote kuondoa hewa, Kanyaga acceleration pedal hadi rpm 2500 wakati mfuniko wa radiator upo wazi hadi uone bubbles za hewa zikitoka kwenye radiator na coolant inazama. Ongeza coolant kidogokidogo ikizama halafu unarudia kubonyeza bonyeza coolant pipes na kukanyaga acceleration hadi air bubbles zinakoma kutoka kwenye radiator.
 
Back
Top Bottom