Isuzu forward haipigi honi wala haishushi kioo

Isuzu forward haipigi honi wala haishushi kioo

Kaluluma

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2019
Posts
468
Reaction score
619
Habari ndugu zangu, nipo na Isuzu

forward hapa

Ina kama siku mbili imesimama

ghafla kupiga honi na kushusha

kioo upande wa dereva.

Nimejaribu kumcheki fundi umeme

wa magari ananiambia shida ya

gari inaweza kuwa kwenye fuse za

gari,

Tumebadili fuse zote lakini bado

changamoto iko palepale

Mwenye ujuzi na hili anisaidie

wakuu.

Natanguliza shukrani [emoji120]
 
Katika vitu hatari kwenye gari ni mfumo wa umeme ukifanya mchezo utaliwasha moto gari lako. Marekebisho ya mfumo wa umeme sio kama kubadilisha tairi au kubadilisha waiper blade. MWITE FUNDI UMEME WA MAGARI MZOEFU AKUREKEBISHIE.
 
Kioo kama hakishuki na kupanda fungua kava kwenye mlango ucheki motor ya power window kama inafanya kazi, kwenye gari kubwa hiyo rubber ya kwenye kioo ikinyauka maji huwa yanapita na kusababisha kutu kwenye motor.

Motor unaweza ukaicheki kama inafanya kazi au haifanyi
 
Honi unatumia aina ipi ya umeme au upepo.

Hizi ndogo za umeme zikipigwa maji huwa zinabadili sauti na kufa, chukua honi nyingine jaribu kama itafanya kazi. Ikigoma mwambie fundi afatilie waya kama umekatika au imepata shoti.
 
Hatimaye kwenye honi nimefanikiwa,
Tatizo bado lipo kwenye kioo
 
Kioo kama hakishuki na kupanda fungua kava kwenye mlango ucheki motor ya power window kama inafanya kazi, kwenye gari kubwa hiyo rubber ya kwenye kioo ikinyauka maji huwa yanapita na kusababisha kutu kwenye motor.

Motor unaweza ukaicheki kama inafanya kazi au haifanyi
Ngoja niichungulie mkuu
,shukrani sana
 
Back
Top Bottom