IT wa HESLB hamko serious na kazi

NEGAN

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2023
Posts
797
Reaction score
1,653
Hii nchi kila kitu ni cha hovyo. HESLB mmefungua dirisha la kuomba mkopo lakini mpaka muda huu watu bado wanaohangaika kukamilisha vipengele.

Mfumo wenu ni mbovu nimelipia control number lakini kila nikitaka ku-create account page ina-load tu tangu asubuhi.

Kama mlijua hamjajipanga kwa nini mlifingua dirisha la maombi.

Pole mkuu, system za kiserikali hovyo kabisa.
 
Ni zaidi ya wiki Sasa tokea nilipie lakini hakuna nilichofanikiwa
 
Hii nchi haijawahi kuwa serious kwa chochote kile kila sehemu watu hawapo serious.
 
Hii nchi haijawahi kuwa serious kwa chochote kile kila sehemu watu hawapo serious.
Huu mfumo mpya wa online waliuoleta walikua na mwaka mzima wa kuujaribu lakini wameamua kukuprupuka. Ni bora wangebaki na mfumo wa zamani tu kama hawajajipanga.
 
Mimi pale kwenye ku-share marafiki eti usubiri hadi bar yote ojae blue, yaani usiku kucha haijajaa. Nimeshindwa ku-dowload form ya dogo
 
Mimi pale kwenye ku-share marafiki eti usubiri hadi bar yote ojae blue, yaani usiku kucha haijajaa. Nimeshindwa ku-dowload form ya dogo
Umeanza mchakato wa kuomba lini. Bora hata wewe unefika step ya mwisho sisi wengine tumekwama step ya kwanza kabisa.
 
Umeanza mchakato wa kuomba lini. Bora hata wewe unefika step ya mwisho sisi wengine tumekwama step ya kwanza kabisa.
Kina Mimi hao najaribu kuload mkoa ninaoishi tu nimekaa siku 4 hakuna mkoa unakuja
 
Kina Mimi hao najaribu kuload mkoa ninaoishi tu nimekaa siku 4 hakuna mkoa unakuja
Mwanzoni nilidhani shida ni browser nikatumia browser nyingine wapi kutumia simu nyingine shida bado ipo.
 
Mkimaliza chuo mtakutana Tena na iyo changamoto kule ajira portal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…