IT wa Tanzania ni "copy-paste" wasioweza kubuni; wanafunzi na wahitimu wote wameshindwa kutengeneza mafaili ya VPN free net?

IT wa Tanzania ni "copy-paste" wasioweza kubuni; wanafunzi na wahitimu wote wameshindwa kutengeneza mafaili ya VPN free net?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Waweza kumfundisha kasuku aseme hana uwezo na ukamzawadia zabibu kumuashiria kafaulu mtihani nae akajiona kichwa, basi ndivyo ilivyo kwa IT wetu wa Tz wanafunzi wa vyuoni na wahitimu kibao, vyeti wanavyo na wengine wana ufaulu mkubwa sana lakini hawana uwezo wa kutatumia maarifa hayo lau kutumia free net kama nchi zingine.

Nchi nyingi masuala ishu za free net ni mambo yanayotatuliwa na jesh la wanafunzi wa IT vyuoni, lakini hapa kwetu mambo ni tofauti sana kiasi kwamba hata wahitimu wanatokewa knockout, mtu ukimwambia akupe hata abcd za pa kuanzia ni mwendo wa kukupa misamiati tu ila vitendo 0
 
Wahenga wanasema debe tupu haliwachi kutika , watu waliofanya makubwa hapa duniani wengi hawana dharau kwa wenzao.
Yaani haiingii akilini jitu linaanza form 5 huku limeshamaliza kusoma topic zote mpaka za form 6.
Huko ni kusoma kwa uelewa au kumeza.
 
Hata maengineer hawajawahi kuvumbua chochote. Hata madaktari sidhani kama kuna chanjo yoyote au dawa wamewahi kuvumbua. Ni janga la kitaifa so unawaonea bure.

Unajua kwann wanashindwa kufanya? Mifumo ya nchi + mifumo ya elimu. Elimu inatengeneza users si creators, and akitokea mtu ame create apewi support kabisa. Anaachwa ku struggle mwenyewe.

Akifanikiwa serikali ndio inajitokeza kupongeza. Unadhani nani atahangaika?
 
So shida yako ni free internet vpn? Why usilipie huduma badala ya kutoa povu?

Likija suala la vumbuzi wapo vijana wanagonga software development vibaya mno, wako kwenye ma kampuni na serikalini.

Ila hawa watu ni wachache mno, the real ones wameshachukuliwa na makampuni they do for profit huko walipo

The rest bado wanahangaika kutafuta kazi
 
lakini hawana uwezo wa kutatumia maarifa hayo lau kutumia free net kama nchi zingine.
Hii Nchi yako ni ya kingese ukifukunyua kuna lidude linaitwa Cybercrime Act na jamàa wanafundishwa Cyber Laws kwamba ukivuka kipengele hiki adhabu ni hii na hii, kufupisha story ukijifanya unachezea mifumo au unabuni mifumo ambayo itaikosesha Serekali mapato kwa njia ya mtandao jiandae aidha kwenda kunyea debe Maisha au ukae nyuma ya Nondo miaka 30+

Akili kumkichwa km wewe upo tayari jaribu tafuta Kali Linux anza kuchokonoa ukidakwa utawaeleza ulikua unatafuta nini, nahitimisha kwa kusema kwenye masuala ya Cyber hii Nchi ni ya kingese imetunga sheria zinazowaba IT wote unaowajua kwa hio usiwaone km mafala.
 
Mafile yakiwepo yannanza uzwa kwa pesa ya maji🤣
 
Mnalaumu bure bila kujua mifumo ya nchi ikoje, mtu anawezaje kufanya innovation zake bila ya kuwa na vifaa vya uhakika? Wapi kuna ICT centers wanapokutana ITs kujadiliana na kufanya innovation zao?
Wapi ITs wanaweza kupata support kwa ideas zao?
 
Mnalaumu bure bila kujua mifumo ya nchi ikoje, mtu anawezaje kufanya innovation zake bila ya kuwa na vifaa vya uhakika?
Wapi kuna ICT centers wanapokutana ITs kujadiliana na kufanya innovation zao?
Wapi ITs wanaweza kupata support kwa ideas zao?
ICT centers jiulize tu kuna kitu kinaitwa bodi ya Tehama ipo ipo tu, mtu unamaliza IT ICT Computer Science inabidi ukasajiriwe kule km kuna michongo na michango uweze kupewa na kuchangia Ila process za kujiunga hazijulikani na wenyewe hawaelezi taratibu zipoje wamekaa kaa tu wanakula kiyoyozi
 
Hata maengineer hawajawahi kuvumbua chochote,
Hata madaktari sidhani kama kuna chanjo yoyote au dawa wamewahi kuvumbua.
Ni janga la kitaifa so unawaonea bure.
Dunia ya sasa ilivyokuwa na maarifa yote ni wewe tu na simu, computer na bando la internet.
Kuna haja ya kumnyooshea mtu kidole kweli?

Msichokijua huwa mnapenda kulaumu watu sana kwa kushindwa kufanya jambo fulani. Tanzania ni nchi masikini na pia ina mfumo mgumu sana wa kupokea hela.

Umetengeneza hiyo program unaiuzaje? Shida mfumo wa malipo, mtu anaamua kufanya mambo mengine tu. Tafuta program inayoitwa Auto CAD au Maya inauzwa shilingi ngapi? Mbongo anaweza kulipa hiyo hela kununua program yako?

Watu wanaoishi nje, unawauziaje mpk hela ikufikie? Shida nyingine. Atengeneze, wewe uje utumie bure au siyo?
 
Back
Top Bottom