Kenya 2022 Itachukua miaka 1,000 Tanzania kufikia chaguzi za Kenya kama tutaendelea kuwa hivi

Kenya 2022 Itachukua miaka 1,000 Tanzania kufikia chaguzi za Kenya kama tutaendelea kuwa hivi

Kenya 2022 General Election
Wa kumlaumu ni Nyerere aliyetengeneza mfumo uliopo
Hakika. Lakini hata Kenya, Zambia, Malawi, Ghana, … waasisi wao waliwarithisha mifumo ya ovyo ya kisiasa. Wao walipambana kuiondoa na kujiletea demokrasia ya kweli.

Sisi kwetu wamekumbatia ushenzi ule wa kale na kuzidi kuhamasisha siasa za kidikteta, manyanyaso na propaganda wakitumia rasilimali za taifa kuunda majeshi ya chawa huku wananchi wakiachwa wazame kwenye giza la ujinga na umasikini uliotopea.
 
Tanzania hatujawahi kuwa na Uchaguzi tangu nchi ipate uhuru bali huwa ni justification tu zinafanyika. Nitamshangaa sana Mtanzania atakayepoteza muda wake kwenye kupiga kura 2025 kwa katiba hii - yaani bora Ulale kama huna la maana la kufanya.
Sasa mkuu hapo umeshauri nini kuhusu jinsi ya kuikabili hiyo hali kama ikiendelea mpaka 2025. I thought you would come up with something advisable, sasa hata tusipoenda kupiga kura ndio CCM watagwaya?!
 
Njia pekee ni Elimu ya Uraia, hadi hapo majority ya raia wa Tanzania watapojua umuhimu wa Katiba. Ni jukumu la kwangu na la kwako - na hiki ndicho wamekuwa wakikifanya vyama vya upinzani atlest leo tumefika walau hapa.

Elimu ya uraia ipo ya kutosha, lakini CCM wanalazimisha kukaa madarakani bila ridhaa ya umma. Kitu pekee kinatufanya watanzania tusifikie viwango vya demokrasia ya Kenya ni kutokutokea machafuko, hivyo CCM wanatuchukulia poa, ndio maana wanaweza kunajisi box la kura kimachomacho.
 
Jamani kila siku napiga kelele nchi nyingi za Africa zimeshaelimika mda sana kwenye uhuru wa demokrasia ikiwemo Zambia, Malawi, Kenya, Ghana na South Africa...
Tatizo CCM ina mafisadi ambao wamejificha nyuma chama, hao ndo wanatufikisha hapa wapo radhi ratibu ratibu michezo ya giza Ili maslahi binafsi yasiguswe, alafu mbaya izo pesa huficha nje wakifa na asilimia kubwa ya pesa hupotea, ila kenya wako mbali.
 
2025 nipo tayari kufa sita kuwa tayari kuona hii rangi ya kinyesi inabeba
Demokrasia ni kushindana kwa uwazi na mshindi halali kutangazwa, na si vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kuhakikisha CCM wanatangaza washindi kwa shuruti.
Na asikwambie mtu kuna raha yake kwamba umekalia kiti KWa kura Halali, inakujengea kujiamini Sana Katika utendaji wake
 
Hapana mkuu bali watu wanataka tume huru ya uchaguzi ambayo itafanya kazi zake pasipo shinikizo la mtu yeyote.

Chaguzi ziwe huru sio mawakala wa vyama pinzani kufungiwa nje ya vyumba vya kuhesabia kura mara polisi kukimbia na mabox ya kura.

Huu ni uoga wa chama tawala ndo maana hawataki tume huru ya uchaguzi.

Unajiuliza kwanini ccm hawataki tume huru ya uchaguzi wakati ni kitu kizuri tu.
Sawa boss, ila Wapinzani wanataka na wapo tayari kupewa nchi au ni wananchi tu wanataka mabadiliko?
Tume kuwa huru ni jambo moja, wapinzani kuwa tayari kupewa madaraka ni jambo lingine, wananchi kuichoka ccm nalo ni jambo jingine.
 
Demokrasia ni kushindana kwa uwazi na mshindi halali kutangazwa, na si vyombo vya dola na tume ya uchaguzi kuhakikisha CCM wanatangaza washindi kwa shuruti.
Na kwa baraka za upinzani. Upinzani na ccm lao moja tofauti ni wananchi tu labda kuna waliochoka jina ccm. Ila hii nchi upinzani=ccm ndo maana ni rahisi kuwa na utulivu panapotokea sintofahamu. Sidhani kama tulitaka kuingia kwenye vyama vingi, Dunia ya wenye nguvu tu imetulazimisha.
 
Nadhani kama watanzania hasa wasomi na wanaopenda kwa dhati maendeleo watakuwa wamejifunza kitu katika mchakato mzima wa uchaguzi kutoka kwa majirani zetu.

It's about time. Zoezi kama hili la sensa ni namna nzuri ya ku-practice matumizi ya digitali kurahisisha mambo, the same iende mpaka kwenye chaguzi zetu.
Tatizo wasomi wetu ni walafi na wabinafsi sana. Wao wanatawaliwa na viongozi wetu ambao wengi ni wabinafsi. So automatically wasomi wetu hawana jipya zaidi ya uchawa
 
Na kwa baraka za upinzani. Upinzani na ccm lao moja tofauti ni wananchi tu labda kuna waliochoka jina ccm. Ila hii nchi upinzani=ccm ndo maana ni rahisi kuwa na utulivu panapotokea sintofahamu. Sidhani kama tulitaka kuingia kwenye vyama vingi, Dunia ya wenye nguvu tu imetulazimisha.

Nyie wazee ndio mnaamini kwenye chama kimoja tena cha CCM, mimi sijawahi kuwa muumini wa siasa za chama kimoja.
 
Sawa boss, ila Wapinzani wanataka na wapo tayari kupewa nchi au ni wananchi tu wanataka mabadiliko?
Tume kuwa huru ni jambo moja, wapinzani kuwa tayari kupewa madaraka ni jambo lingine, wananchi kuichoka ccm nalo ni jambo jingine.

Kwa taarifa yako, chama au mtu yoyote mwenye akili timamu anaweza kuwa kiongozi wa nchi hii. Kazi aliyoweza JK na Magufuli nani atashindwa? Hiyo mitazamo ya kusema eti wapinzani hawajawa tayari kupewa nchi, hutolewa na wanaccm kama Hadaa kwa umma, na kuhofia kupoteza madaraka.

Na jambo hilo hutekelezwa na kundi lijiitalo system, wengi wa hawa ni viongozi wastaafu wa serekali, vyombo vya ulinzi na usalama na wale walioko madarakani sasa. Hawa huogopa CCM kupoteza madaraka kwani ndio inayowahakikishia ulaji kwakuwa wanaendelea kulipwa hadi wafariki, hawana uhakika wa kuendelea kula keki ya taifa iwapo wapinzani wataingia madarakani. Njia pekee ya kuondoa huu uhuni ni machafuko, ama nchi kupinduliwa tuanze upya kwenye mifumo ya kiutawala.
 
Back
Top Bottom