Tila-lila2
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 652
- 1,058
Ni wazi kuwa Benard Membe anaenda upinzani. Mkakati unakamilika tarehe 21 Julai, 2020. Tukae mkao wa mapambano!
Katika inayotarajiwa kuwa hotuba yake Benard Membe anaelezwa kuleta picha kubwa zaidi ya inavyofikirika katika kambi ya upinzani. Katika maelezo yake ataanza na kuelezea kuwa katika maisha yake yote ya kisiasa hakuwahi kushambuliana na wanasiasa wenzake, si wa upinzani wala wa ndani ya Chama chake. Yeye amekuwa ni mtu wa kujitetea tu siku zote. Amekuwa akishambuliwa bila sababu yeyote.
Ataeleza jinsi anavyoamini katika mshikamo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kidemokrasia. Ateleza namna kipato cha kila mtu kilivyopomoroka kwa kipindi hiki cha miaka mitano na yeye atakavyokuja na sera mbadala ya kuwajaza wananchi na njururu. Hapo atakugusia kupomoroka kwa kipato cha wafanyakazi na kupanda chati ya kimaslahi kwa wale wateule wa Mkulu wanaopendelewa. Atatoa ushahidi, pay roll inayoonesha Doto James kulipwa siku 6 kwa kazi ambayo hajashiriki hata kidogo. Ana huo ushahidhi tayari.
Katika hotuba yake ataonesha namna gani wapinzani wana nguvu wakiwa pamoja na kusisitiza upendo kwa nchi yetu. Ataeleza kwa kukosoa jinsi nchi inavyoongozwa kwa ubabe kwa sasa wakati hakuna hata haja ya kuleta ubabe usio na maana. Ataongelea kuhusu kuminywa kwa demokrasia akigusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ataongelea kupotea kwa watu na kuminywa kwa uhuru wa habari. Ataongelea jinsi hali za kipato kwa wananchi zilivyo hafifu na kukosoa ujenzi wa miundo mbinu ambayo haina manufaa yeyote kwa kipato cha mwananchi wa kawaida. Pamoja na kuwa jana Tanzania imetangazwa nchi iliyohamishiwa kwenye kundi la nchi za kipato cha chini bado wananchi hawatakuwa na manufaa yeyote kwa sababu kuhamishiwa huko ina maana kuwa nchi itakuwa inakopesheka na haitakuwa ikipata misaada tena.
Ataongea kuhusu umuhimu wa Katiba mpya na kuahidi kutenganisha majukumu ya wakurugenzi kusimamia Uchaguzi kwani wanakuwa nao ni sehemu ya Tume ya Uchaguzi. Ataeleza kwa kina kuwa kuanzia ngazi ya chini kabisa atatengeneza mazingira ya uhuru wa wananchi wa chini kuchagua viongozi wao. Ataeleza kuwa wananchi kuanzia ngazi za chini waishi kwa kupendana na wasijengewe chuki na watawala kwa ajili ya watawala kutaka kutawala kwa nguvu. Ataahidi kuondoa kinga ya kutoshtakiwa kwa Rais na viongozi wengine akielezea kwa kina kuwa Serikali itayaoingia madarakani haitakuwa na sababu za kujiwekea makinga kinga wa sababu itakuwa ni Serikali safi.
Ataahidi kulipa fidia kwa wale waliobomolewa nyumba zao Dar na kwingineko. Ataahidi kuendeleza Jiji la Dodoma kwani anaufahamu Mpango Kazi wote kuhusu kuendeleza mji huo. Ataahidi kuwafanyia wafanyabiashara mazingira rafiki ya kufanya biashara zao ikiwepo kutowabambikizia kodi bila utaratibu unaoeleweka. Ataahidi kuanzisha uchunguzi kuhusu matukio ya watu kupotea na wale waliomtwanga risasi Tundu Lisu akionesha kwa wazi kuwa watu hao watapatikana iwe isiwe.