Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SUBIRI KAKA,SISI TUNAGOMBEA NA MVUTO WETU UTAUONA, time will tellKitu pekee tu nilichokigundua kwa haraka ni kwamba Membe ana Washauri Wapuuzi na Wanafiki sana ambao nina uhakika wanampoteza mazima na wanamtafutia matatizo ambayo bahati nzuri hata Yeye Mwenyewe ( Membe ) kwa Kiapo chake anayajua kuwa akiyakiuka yatamgharimu tu.
Bado sijauona huo Mvuto wa Kisiasa alionao Membe hata kama akiungana na huyo Kiongozi wa Wanasiasa Wanafiki Tanzania nzima. Anajisumbua bure tu!
Yani Kama na uchaguzi ujao upinzani ukiungana halfu ukampitisha kada wa CCM alietimuliwa ndo awe mgombea urais ndo nitaamini kabisa kuwa Tanzania bado hakuna upinzan wa kweli Bali Kuna Wahuni tu.
Yeyote atakayekuwa anagombea dhidi ya jiwe la chattle basi ajue ana kura zetu wabongo 95%.Ni wazi kuwa Benard Membe anaenda upinzani. Mkakati unakamilika tarehe 21 Julai, 2020. Tukae mkao wa mapambano!
Katika inayotarajiwa kuwa hotuba yake Benard Membe anaelezwa kuleta picha kubwa zaidi ya inavyofikirika katika kambi ya upinzani. Katika maelezo yake ataanza na kuelezea kuwa katika maisha yake yote ya kisiasa hakuwahi kushambuliana na wanasiasa wenzake, si wa upinzani wala wa ndani ya Chama chake. Yeye amekuwa ni mtu wa kujitetea tu siku zote. Amekuwa akishambuliwa bila sababu yeyote.
Ataeleza jinsi anavyoamini katika mshikamo katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kidemokrasia. Ateleza namna kipato cha kila mtu kilivyopomoroka kwa kipindi hiki cha miaka mitano na yeye atakavyokuja na sera mbadala ya kuwajaza wananchi na njururu. Hapo atakugusia kupomoroka kwa kipato cha wafanyakazi na kupanda chati ya kimaslahi kwa wale wateule wa Mkulu wanaopendelewa. Atatoa ushahidi, pay roll inayoonesha Doto James kulipwa siku 6 kwa kazi ambayo hajashiriki hata kidogo. Ana huo ushahidhi tayari.
Katika hotuba yake ataonesha namna gani wapinzani wana nguvu wakiwa pamoja na kusisitiza upendo kwa nchi yetu. Ataeleza kwa kukosoa jinsi nchi inavyoongozwa kwa ubabe kwa sasa wakati hakuna hata haja ya kuleta ubabe usio na maana. Ataongelea kuhusu kuminywa kwa demokrasia akigusia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ataongelea kupotea kwa watu na kuminywa kwa uhuru wa habari. Ataongelea jinsi hali za kipata kwa wananchi zilivyo hafifu na kukosoa ujenzi wa miundo mbinu ambayo haina manufaa yeyote kwa kipato cha mwananchi wa kawaida. Ataongelea kuhusu kutofuatwa kwa sheria na upendeleo wa waziwazi unaoneshwa na Serikali hii.
Ataongea kuhusu umuhimu wa Katiba mpya na kuahidi kutenganisha majukumu ya wakurugenzi kusimamia Uchaguzi kwani wanakuwa nao ni sehemu ya Tume ya Uchaguzi. Ataeleza kwa kina kuwa kuanzia ngazi ya chini kabisa atatengeneza mazingira ya uhuru wa wananchi wa chini kuchagua viongozi wao. Ataeleza kuwa wananchi kuanzia ngazi za chini waishi kwa kupendana na wasijengewe chuki na watawala kwa ajili ya watawala kutaka kutawala kwa nguvu. Ataahidi kuondoa kinga ya kutoshtakiwa kwa Rais na viongozi wengine akielezea kwa kina kuwa Serikali itayaoingia madarakani haitakuwa na sababu za kujiwekea makinga kinga wa sababu itakuwa ni Serikali safi.
Ataahidi kulipa fidia kwa wale waliobomolewa nyumba zao Dar na kwingineko. Ataahidi kuendeleza Jiji la Dodoma kwani anaufahamu Mpango Kazi wote kuhusu kuendeleza mji huo. Ataahidi kuwafanyia wafanyabiashara mazingira rafiki ya kufanya biashara zao ikiwepo kutowabambikizia kodi bila utaratibu unaoeleweka. Ataahidi kuanzisha uchunguzi kuhusu matukio ya watu kupotea na wale waliomtwanga risasi Tundu Lisu akionesha kwa wazi kuwa watu hao watapatikana iwe isiwe.
Ni Membe Mwenewe ID KibaoKumbe wewe Ni nabii
Mkuu hata Membe apange sentensi tamu za kuvuta wapinzani namna gani, kilichotokea kwa Lowassa kinatosha. Wengi wetu hatuko tayari tena kurudia kosa. Kama anakuja upinzani kudai tume huru ya uchaguzi hapo ni sawa, ila sio apewe nafasi ya kugombea urais kisha tumuunge mkono. Tunajitambua vya kutosha.
Zitto amekwisha mkaribisha.
Anaruhusiwa kwa 100%, lakini asitarajie wapinzani wanaojitambua kumuunga mkono huyo mzee wa ccm. Somo tulillolipata kwa Lowassa linatosha. Kutenda kosa sio kosa, bali kurudia kosa.
Nadhani ACT haijatangaza fomu za urais ili kumsubiri subiri.
Yeyote atakayekuwa anagombea dhidi ya jiwe la chattle basi ajue ana kura zetu wabongo 95%.
Atueleze tu mkakati utakaotumika pale wahuni watakapogoma kukabidhi ushindi wetu kama ambavyo wamekuwa wakifanya hapo awali.
Maana haiwezekani toka 95 napiga kura mpaka leo kushinda mnashinda kila mara, mnaporwa ushindi hamchukui hatua za kuonekana
Chadema mchukueni awe mgombea wenu. Kauli yake so mnaijua? Kazi na Bata! Ahahahahah!Inakuwaje unawadharau wenzako kiasi hata unawaita wapuuzi? Nani kakudanganya kuwa wewe ndiye genius?
Wacha dharau na huo u genius wako baki nao nyumbani kwenu.
Chadema mchukueni awe mgombea wenu. Kauli yake so mnaijua? Kazi na Bata! Ahahahahah!
CCM ina wenyewe na Membe sio sehemu ya wenyewe.Membe kesha jiandaa kwenda kuchukua form wiki hii hapo lumumba
Ikijirudia tena Upinzani hautakuwa na maana Tena na Kazi yetu wapiga kura tutawapuuza tu na kuendelea kuiamini CCM ambayo inaonekana kurejea kwenye msitari wa Maendeleo ya kweli.Na kisipotokea hicho mkuu kwa chadema ama Act mkuu nidai bia 5...
Miaka mi5 hakuna mkakati wa kuandaa mgombea na kumpika...
Last minute wanachukua most popular.. aliyetoka ccm...
Watajitetea "tutamtumia hata shetani kuitoa CCM madarakani".
Umenena!Yeyote atakayekuwa anagombea dhidi ya jiwe la chattle basi ajue ana kura zetu wabongo 95%.
Atueleze tu mkakati utakaotumika pale wahuni watakapogoma kukabidhi ushindi wetu kama ambavyo wamekuwa wakifanya hapo awali.
Maana haiwezekani toka 95 napiga kura mpaka leo kushinda mnashinda kila mara, mnaporwa ushindi hamchukui hatua za kuonekana