Itakuaje siku Diamond akiwaomba radhi clouds TV?

Lazima atakuja kuenda kuomba msamaha Unajua Tatizo kubwa ni kwamba mashabiki wanamjaza upepo Diamond anasahau Clouds wamempa Airtime kubwa sana sio Busara kwa meneja kuanza kurusha madongo mitandaoni wakati hayana ukweli
 

Dimondi ni Overrated musician,na wanafanya hivyo kusudi ili apate dau kubwa kwenye shows,aonekana expensive.
 
Mange kashawacheulia huko.


Wanamuamini zaidi ya misaafu..

Mwanaume mzima anakuja hapa na vigelegele eti mange kakinukisha!!???

Aisee tumetofautiana sana
wanaume wa aina iyo niwale wanaopumuliwa
 
itajulikana tuu nani yupo jumba la vioo halafu anavugumisha mawe.....kwa ugomvi..???
 
Amna lolote kama ana amua kuanzisha radio natv yake ata weza tuuu kwani uyo kusaga kawezaje na ao wcb watashindwaje nimbinu tu zabiashara mambo yatajipa

Ila samahani , usinielewe vibaya.
Jifunze kuandika. Maneno mengi uliyoandika sio sahihi. Acha kuharibu lugha.
Siku njema.
 
Hivi kumiliki Radio na TV,inahitaji uwe trillion ngapi na akili kubwa kiasi gani ,naomba mafundi wa haya mambo mnifahamishe.
 
Kwa nini isiwe "itakuwaje siku Clouds wakimuomba radhi Diamond?"
 
Ila kuendesha Radio/Tv si kazi rahisi. Mpaka upate mashabiki royal inahitaji muda sana.
Na radio si Muziki tu, siku hizi Watu wanapata Muziki wanapata Youtube na social networks nyingine. Radio/Tv zinahitaji contents tofautitofauti na kusoma mahitaji ya soko.

Cc: chige
TRUE, media yoyote... sio TV na radio peke yake bali hata gazeti na blog!!

Ingawaje watu wanaona ni kama kitu kinachohitaji mabilioni lakini ukweli ni kwamba kuanzisha TV/Radio sio kazi but kinachofuata; yaani Content ndio mtihani mgumu kuliko starting capital!

Hata hivyo, Diamond ana advantage moja compared na watu wengine! Pale alipo tayari ana angalau 1 million Viewers/Listeners wanaosubiri tu kubonyeza kitufe!

Changamoto pekee kwake ni kuhakikisha wale wanaosubiria kubonyeza kitufe wanarudi tena na tena kwenye kitufe baada ya kuwa wamebonyeza kwa mara ya kwanza!

Hapo ndipo linakuja suala la content ambalo ndio determinant la number and type of audience including audience loyalty!
 
1.Hivi kwa nn kila msanii anapokuwa yupo ktk peak analalamika clouds fm wanamwibia?
2.Nitajieni msanii ambaye aliyesimamiwa na clouds, ambaye financial yupo stable?
Mimi mtizamo wangu naona clouds wanaongoza kutengeneza WASANII MASIKINI WENYE MAJINA MAKUBWA, mf Barnaba (msanii wa bongo fleva aliyekamilika anatunga na kuwatungia wenzake, anapiga gita na ana vocal kali) hana cha maana zaidi ya sifa na promo anazopewa na clouds. Mimi diamond nampongeza kwani anajua hatokuwa namba moja milele na ndio maana ameamua kuwekeza na kuhakikisha kila anachokifanya kinamuingizia ela. Bila kusahau hawa hawa clouds ukifilisika kimziki na kifedha wanaanza kukudharau na kukucheka ktk SHILAWADU.
 
ila diamond hana hela maisha yake ni maigizo na huu mwaka kauanza vibaya sana
 
Kuna Tv na radio nyingi mno hazipati faida TZ..na zina pesa
mfano TV ya David Mosha....haina hata watazamaji licha ya mtaji mkubwa
ASTV..

Ndo naiskia leo hiyo TV, aiweke dstv or Azam tv
 
Amna lolote kama ana amua kuanzisha radio natv yake ata weza tuuu kwani uyo kusaga kawezaje na ao wcb watashindwaje nimbinu tu zabiashara mambo yatajipa

Clouds ni kama ITV, walianza zamani pia commercial radio zilikuwa kati ya 5 au 10. Leo zipo zaidi ya 100.

Ilikuwa rahisi kutoboa wakati ule kuliko sasa.
 
Mbona mnapenda kutoa mifano ya watu waliofeli? kila mtu ana mbinu zake ww kusoma ujui ata picha uoni? huku mtaani ni wasafi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…