Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni Taasisi kubwa sana , si Taasisi inayoweza kutumika Kisiasa kama anavyotaka kufanya RC wa Dar es Salaam , Albert Chalamila , ama Chalamila hajui mipaka ya Cheo Chake au analeta Usanii wake uliozoeleka , Bali ninachokijua ni Kwamba Chalamila ameropoka bila ku consult kiongozi yeyote wa juu .
Jeshi la Wananchi haliwezI kutii maagiizo ya kijinga kutoka kwa kiongozi wa chini kama Mkuu wa Mkoa , linaweza kutii maagizo ya Rais , Waziri wa Ulinzi au Mkuu wa Majeshi , Tuliwahi kumkataza Mkuu mmoja wa Wilaya Humu kuacha kuvaa sare za Jeshi kwenye shughuli zake (Tunashukuru kwamba alituelewa )
Kwahiyo nachukua nafasi hii kumkumbusha ndugu Chalamila kwamba hana mamlaka yoyote yale ya kuliamrisha Jeshi la Wananchi katika jambo lolote lile , kwanza anapaswa kuwajibika kwa kujiuzulu kutokana na dharau kwa JW kwa kulipa kazi ya kusafisha mitaro , hii si kazi ya JW , vinginevyo atueleze hawa Wakandarasi wazoa taka wanaolipwa hela nyingi na Wananchi wapo kwa ajili ya nini .
Natoa wito kwa viongozi wa chini kama hawa Wakuu wa Mikoa kuacha kukwepa hoja za kisiasa na kujificha kwenye majeshi yetu , Huo ni Udhalilishaji , Sisi wananchi hatutakubali .
View attachment 2870893