Itakuwa jambo jema na la busara kama Serikali ya Tanzania itaifungia Twitter

Itakuwa jambo jema na la busara kama Serikali ya Tanzania itaifungia Twitter

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Hakuna ubishi kabisa watu wengi wanaoneza uongo juu ya Taifa letu ni watumiaji wa mtandao wa Twitter.

Huko kuna watu wabaya sana ambao nafikiri sababu wengi wao wanaishi nje ya nchi basi muda wote ni kueneza propaganda za uongo na kutukana viongozi.

Mbona China waliifungia baada ya kuona inahatarisha usalama wa nchi yao? Maana watu wanatengeneza picha za uongo ili kuleta chuki dhidi ya serikali haifai kabisa kwa Tanzania.

Mfano hata kama mtu amepigwa risasi hivi kweli risasi inaweza kutoboa kifua cha mtu tundu la nchi nne?

Wengi wa hawa watu wanaotukana viongozi wapo nje ya nchi, wanatukana viongozi na kupotosha umma juu ya masuala mengi tu,hata kipindi Covid 19 inaingia Tanzania walipotosha watu kwa uongo mwingi na kutengeneza video za uongo.

Kwa hiyo serikali sikivu ya CCM ifunge Twitter maana siku za usoni italeta balaa kwenye nchi yetu.

Leo sina mengi najua litafanyiwa kazi na sasa naenda kijiweni kunywa kahawa na Alikasusu. Nafikiri wadau kijiwe mnakifahamu.
 
Serikali ya awamu ya 5 imepoteza uhalali wa kuiongoza nchi. Haijachaguliwa kihalali. Ndiyo Serikali ya kwanza itayotinga ICC tangu tupate Uhuru. Kwanini isikolewe mitandaoni?

Hata wakifunga mitandao yote, bado teknolojia itawapa fursa wenye uchungu kutumia VPN na mawasiliano yataendelea kama kawaida. Be broad minded please. Acha ujinga zama hizi.
 
Kijiwe kiko wapi mkuu wangu?

Hapo Barabara ya kupandisha kutoka Alimaua?

Ama hicho hapo Makumbusho Stendi karibu na MALIWATO ya kulipia ya stendi?!!!

Mkuu kule TWITTER kuna mambo banaa hatareee.....

Yaani kuna jitu linaitwa KIGOGO 2014 daah hili sijui HALIROGEKI?!?
Eti ninasikia linatembea na mifupa ya nguruwe maana hata Ahlulbadiri aliyotandikwa na "sheikh" wangu MZITO wiki iliyopita imemrudi MWENYEWE maalimu wangu HUYO wa pale Se......i kwani jana AMENIJULISHA kupigana na CHATU MWEUSI usingizini na ameamka HOI.

Maalim Uwesu J. wa pale Buza kwa.......amemfanyia RAMLI na kugundua kuwa eti ni MAJINI 500 YA hili LiKIGOGO 2014 ndiyo YALIYOMBEEP sheikh wangu HUYO.

Hapa niko mtatizoni yaani sijajua huyo bwana ni BINADAMU Kama sisi ama Jini Mjukuu wa Ifrit mkaa baharini loooh

Mshana Jr njoo tafadhali.
Kitoabu please nawe uje.
 
Wakati ukionyesha 'Chuki' za wazi wazi Kwao 'Twitter' na kutaka 'Serikali' iifungie tambua kuwa hata Rais wako JPM nae ni mwana 'Twita' vile vile.
Kuwa JPM anatumia Twitter sio sababu ya kuruhusu upuuzi ,matusi, na upotoshaji wa watu wanaokaa ughaibuni. Aachane na Twitter kama ni salamu awe au jambo lolote atumie njia za kiofisi, Twitter sio official.
 
Subirini kipindi cha haramu nyingine, mkifanya hivyo wakati huu haita noga.
 
Si jambo rahisi kufunga tu twitter na mitandao mingine.

Ni suala la kiufundi sana na siwezi kulizungumzia kwa undani kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa taifa.

Ila inawezekana, na hao China na nchi zingine kadhaa zimeweza kutofunga bali kwa kutumia njia kadhaa ikiwemo ya kuwasiliana na huduma za internet yaani ISPs na wale wa binafsi kama wa VPN, ambapo kunawekwa sera kadha wa kadha.

Kinachotafutwa ni kuweka balance kati ya masuala ya kueneza sumu mitandaoni na nia njema ya watumiaji wa mitandao hiyo.
 
Back
Top Bottom