Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Mjadala ulioibuka baada ya Janabi kupendekezwa kuingia katika ushindani wa kugombea nafasi ya Mkurugenzi wa WHO kanda ya Africa ni muhimu ila umepotoka kiasi kikubwa kwa kushindwa kujikita katika mahitaji ya mtu anayetakiwa katika hiyo nafasi. Pamoja na hayo nakubiliana na wanaosema CV ya Janabi inaweza isitoshe katika hiyo nafasi ila kwa vigezo tofauti na muhimu anavyokosa pamoja na kwamba yeye ni dakatri gwiji na bingwa.
Mtu anayehitajika katika nafasi hiyo ni mwenye uzoefu wa sera za afya, uongozi katika afya ya umma(public health) na zaidi sana ubobevu katika masuala ya magonjwa ya kuambukiza na milipuko. Haya ndio mambo kipaumbele kwa nafasi kama hiyo, sio gwiji wa matibabu au daktari bingwa. Ndugulile aliipata hiyo nafasi akiwa sio daktari gwiji au bingwa, wakuregenzi wengi WHO sio madaktari bingwa au magwiji wa matibabu na hata Mkuregenzi mkuu wa sasa wa WHO sio daktari kabisa kwa taaluma. Janabi anakosa sifa na uzoefu mkubwa katika maeneo haya yote.