Showio
JF-Expert Member
- May 16, 2019
- 254
- 482
Hata siku moja mti au mmea hauchagui aina ya tunda la kuzaa. Muembe hauchagui kuzaa embe au zambarau ni lazima muembe uzae embe.
Mchungwa hauna option ya kuchagua kuzaa chungwa au chenza, nilazima utazaa chungwa kwasababu hiyo ndio asili yake na ndivyo lilivyokuwa designed na aliyeliumba.
Kuna hali kwenye maisha ukishakuwa nayo basi automaticaly matokeo yake ni dhahiri na lazima. Kuna tabia ukishajijengea basi matokeo yake ni hakika.
Huwezi kuwa na asili ya uvivu halafu ukafanikiwa, hata siku moja, kama ambavyo nyanya chungu haiwezi kuzaa nyanya ya kawaida. Never. Huwezi kuwa mmbea na mhamisha maneno ukapendwa na wengi, la hasha.
Unapotaka kuwa na tunda la urafiki wawengi lazima uhakikishe wewe ni mti wenye tabia kamavile upole, mkweli, muaminifu, mkarimu nk.
Mara nyingi wengi tunalalamika sana vitu haviendi vile tunavyotaka, jiulize je matokeo unayoyataka yanaendana na asili yako? Kama unataka tunda fulani basi kuwa mti wake.