Itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
[Luk4:1]Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani
[Mat4:8]Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake
[Luk4:6]Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.
[Luk4:7]Basi, wewe ukisujudu mbele yangu yote yatakuwa yako.
[Luk4:8]Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
[Mark8:36]Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
 
Kichwa cha habari tu kimenibariki
 
Hasara ya nafsi ni chuki, hasira, kukata tamaa, wivu, tamaa mbaya mwisho ni kukoswa aman ya moyo na furaha ya maisha
 
Yataka moyo bila kuongozwa na roho wa bwana ni ngumu kweli.Binadamu wanampenda Mungu sema tu subira na majaribu ndio vinatufanya tuchukue njia za mkato na Mungu yupo kwa wenye kusubiri kwakua mipango yetu si yake na mipango yake si yetu

Hutenda kwa wakati wake.Subira ni muhimu sana tofauti na hapo mbona shetani anakupata tu
 
Ni kweli mtumishi! Peke yetu hatuwezi kumshinda Shetani. Tunahitaji neema kuungojea wakati wa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…