Itel gado ofa toka vodacom ni utapeli

Itel gado ofa toka vodacom ni utapeli

IQup

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2018
Posts
1,166
Reaction score
1,808
Ndugu yeyote mwenye uhitaji wa simu hiyo ambayo vodacom wanajinadi kuwa ni OFA na kuiuza kwa bei ya elfu95. Hiyo Itel gado yao ndani wanaeleza kwamba "utapata GB 3 kila mwezi kwa miezi 4 BURE". Hiyo ofa ya internet ni waongo wanadanganya umma, wanatoa miezi miwili tu na kusitisha hiyo huduma, kwahiyo wanunuzi ambao mnataka kununua hizo simu angalia usijefurahishwa na gb 3 ...utaumia, jipange kwa kuridhika na sifa zingine tu. Hao wanajitangaza sana na hiyo simu yao ila wanafeli kukamilisha hicho walichokisema, ukinunua unakuwa umewapunguzia stock na wanakusitishia internet kabla ya muda unaotakiwa

Mimi nimenunua simu yao moja, wakaniungasha mwezi huo na unaofuata baasi, wakatokomea. Baada ya hapo wamekuwa kimya, nimewafatilia hadi makao makuu(kwa njia ya email) lakini wanatoa majibu ya kihuni sana, kwa tafsiri ya wazi ni kwamba simu haitapewa tena gb zilizosalia, hata nilipoenda vodashop nilipoinunulia hiyo simu nao ni wahuni tu kama wale wa makao makuu (majibu yao ni ya kijanja janja ..utapelitapeli). Wanaishika shika simu wanatuma sms wanasema subiri utapokea, nishawasumbua sana lakini kila siku wanajibu subiri, so utasubiri hadi miezi iliyosalia iishe. Wanunuzi kuweni makini na ofa!!!

Nunua hiyo simu SIO kwa kigezo cha internet wanayojitangaza nayo kwenye vyombo vya habari.
IMG_20180915_093042.jpg
 
Kitonga?!😁😁
Hapana Boss, hizi ni ofa ambazo wauzaji hawawezi kutekeleza kile wanachokisema. Wala sio kitonga, package yao ni uongo na uizi
 
Sasa kiongozi yaani ununue simu sababu kubwa iwe ni bando ya bure?
Kweli yajayo yanafurahisha.
 
Hiyo ni mojawapo ya huduma ambayo wameahidi watakupatia, huo ni kama mkataba wa kimaneno baina ya mnunuzi na muuzaji. na mimi kweli nilitaka nitumie internet ikiisha ofa nimpe mtu simu kama zawadi yake. Wamenivunja nguvu kabisa hawa wezi Vodacom
 
Pole mdau kwa tatizo lililokupata,

Tunaomba mawasiliano yako PM kwa ufuatiliaji na utatuzi wa shida hii.

Karibu sana.
Sawa nashukuru, kuna email zangu nyingi sana mnazo mmezijibu bila mafanikio. rejeeni email alizokuwa anajibu bwana mwaijele lwimiko (Hilo ni jina la kwenye email). email ya mwisho ya lalamiko hili ni email ya tarehe 5 Sept 2018. Fuatilia hii taarifa alafu rejeshea hapa hapa majibu, wala sio huko PM
 
Ahahahahahaaa mkuu kumbe hii ni dawa, ni kuwatangaza tu hakuna njia nyingine.
Wanafanya ujanja ujanja huko wanadhani hakuna pa kusemea, sisi popote tutasemea tu ili na wengine kabla hawajaamua kununua wajue haya wanayoyafanya
 
Ndugu yeyote mwenye uhitaji wa simu hiyo ambayo vodacom wanajinadi kuwa ni OFA na kuiuza kwa bei ya elfu95. Hiyo Itel gado yao ndani wanaeleza kwamba "utapata GB 3 kila mwezi kwa miezi 4 BURE". Hiyo ofa ya internet ni waongo wanadanganya umma, wanatoa miezi miwili tu na kusitisha hiyo huduma, kwahiyo wanunuzi ambao mnataka kununua hizo simu angalia usijefurahishwa na gb 3 ...utaumia, jipange kwa kuridhika na sifa zingine tu. Hao wanajitangaza sana na hiyo simu yao ila wanafeli kukamilisha hicho walichokisema, ukinunua unakuwa umewapunguzia stock na wanakusitishia internet kabla ya muda unaotakiwa

Mimi nimenunua simu yao moja, wakaniungasha mwezi huo na unaofuata baasi, wakatokomea. Baada ya hapo wamekuwa kimya, nimewafatilia hadi makao makuu(kwa njia ya email) lakini wanatoa majibu ya kihuni sana, kwa tafsiri ya wazi ni kwamba simu haitapewa tena gb zilizosalia, hata nilipoenda vodashop nilipoinunulia hiyo simu nao ni wahuni tu kama wale wa makao makuu (majibu yao ni ya kijanja janja ..utapelitapeli). Wanaishika shika simu wanatuma sms wanasema subiri utapokea, nishawasumbua sana lakini kila siku wanajibu subiri, so utasubiri hadi miezi iliyosalia iishe. Wanunuzi kuweni makini na ofa!!!

Nunua hiyo simu SIO kwa kigezo cha internet wanayojitangaza nayo kwenye vyombo vya habari.
View attachment 866666
Nasikitika sana kuona mtu anatoa pesa yake na kununua Infinix,Itel ama Tecno
 
Back
Top Bottom