Ndugu yeyote mwenye uhitaji wa simu hiyo ambayo vodacom wanajinadi kuwa ni OFA na kuiuza kwa bei ya elfu95. Hiyo Itel gado yao ndani wanaeleza kwamba "utapata GB 3 kila mwezi kwa miezi 4 BURE". Hiyo ofa ya internet ni waongo wanadanganya umma, wanatoa miezi miwili tu na kusitisha hiyo huduma, kwahiyo wanunuzi ambao mnataka kununua hizo simu angalia usijefurahishwa na gb 3 ...utaumia, jipange kwa kuridhika na sifa zingine tu. Hao wanajitangaza sana na hiyo simu yao ila wanafeli kukamilisha hicho walichokisema, ukinunua unakuwa umewapunguzia stock na wanakusitishia internet kabla ya muda unaotakiwa
Mimi nimenunua simu yao moja, wakaniungasha mwezi huo na unaofuata baasi, wakatokomea. Baada ya hapo wamekuwa kimya, nimewafatilia hadi makao makuu(kwa njia ya email) lakini wanatoa majibu ya kihuni sana, kwa tafsiri ya wazi ni kwamba simu haitapewa tena gb zilizosalia, hata nilipoenda vodashop nilipoinunulia hiyo simu nao ni wahuni tu kama wale wa makao makuu (majibu yao ni ya kijanja janja ..utapelitapeli). Wanaishika shika simu wanatuma sms wanasema subiri utapokea, nishawasumbua sana lakini kila siku wanajibu subiri, so utasubiri hadi miezi iliyosalia iishe. Wanunuzi kuweni makini na ofa!!!
Nunua hiyo simu SIO kwa kigezo cha internet wanayojitangaza nayo kwenye vyombo vya habari.