Mojawapo ya mambo yanayozisaidia jamii kupiga hatua ya maendeleo ni pamoja na kujali muda.Naangalia tamasha la bulabo lililopo live TBC.Kila kiongozi anayepanda kuanza kuzungumza,anataja itifaki ya viongozi waliopo.Muda unapotea sana kabla hata mgeni rasmi hajaanza kuzungumza.Sisi kama taifa,hatuwez kweli kuwa tunafupisha kutaja taja majina na kujikita katika lengo lililotukutanisha?Kuna sehemu nilialikwa ktk uzinduzi wa choo,zilipotea dakika zaidi ya 10 za viongoz kutaja tu itifaki.Wataalamu naomba mtusaidie au mshauri uwezekano wa kufupisha hotuba au kukaribisha kila mtu aje kusalimia au kutoa neno.Tukizingatia muda kwa kila tunachokifanya ikiwemo muda wa kuingia kazini na kutoka,tutafika mbali.