Itikafu=ITIQAF.Neno hilo ni lakabu ya kiarabu. Itiqaf, ni ile hali ukaayo mahsusi kumuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu juu ya yote yanayokusibu au kuomba msaada. Mara nyingi Itiqaf hufanyika katika zile siku 10 za mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Ambapo wachamungu wa kweli hukaa misikitini pasipo kujihusisha na masuala mengine yeyote ya kimaisha au kidunia wala kuongea na waaminio waingiao kusali zaidi ya 'Assalaam alaikhum' pekee. Kwamba waaminio wanaokaa Itiqaf basi muda wao wooote wa hizo siku 10 hutumika katika ibada tu, yaani kuongea na Mwenyezi Mungu tu. Mwisho huwa ni mwezi unapoandama na kuthibitishwa kuwa siku inayofuata ni Eid.JK amechanganya mambo, kuna kitu huitwa 'MUBAHALA'. Mubahala ndio hutumika rasmi kuamua NGUVU ya Muumba ichukue hatua. Tena Mubahala huwa ni wazi ambapo mshitaki na mshitakiwa wote hupeana taarifa rasmi (kubainisha muongo na mkweli), (apokelewaye dua na asiyepokelewa dua). Mubahala hutoa idadi ya siku maalum hukumu ya Muumba kuwa imetolewa.JK kachanganya kati ya 'itiqaf' na 'mubahala', anapaswa aingiliapo masuala ya dini awahusishe wanazuoni wa kiislam kumpatia tafsiri yenye tafsida nzuri kwa umma.Rock City.