ITIKAFU ni nini?

ITIKAFU ni nini?

Status
Not open for further replies.
Mm binafsi bado namuombea uhai sana Jakaya Mrisho Kikwete, ili baada ya mwaka 2015 ana mshtaka ya kujibu, lazima apande mahakamani, sema hawa wanaitikafu wanataka kutupeperushia ndege wetu!
1.kudanganya WA -TZ kuwa atawapa maisha bora!
2.Kuua raia wema wakiandamana kudai Haki.
3.Kushindwa kusaidia ulinzi wa raia na mali zao! as per katiba!
 
Huyu ------ sijui kweli ni Muislam au kanyaboya tu!! Kuna uhusiano gani kati ya ITIQAF na kuombewa adhabu kwa Mungu? Alikuwa anamaanisha AL BADR au nini? ITIQAF ni ibada inayofanyika kwenye kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhan kuomba maghafillah(msamaha na kumtaka Mungu akunyooshee mahitaji yako), sasa inauhusiano gani na yeye kuombewa afe?

Kumbe jamaa ni dhaifu hadi kwenye dini yake duh!Kweli ni janga la dunia!!
Kanyaboya tu?, mkuu, japo nimeipenda hiyo lakini nimecheka sana
 
Japo huyo uliemnukuu mie simwamini kabisa!...
Ila naomba niuleza swali, kumwombea mtu kifo..sio kati ya haya? (ile haombi mambo ya madhambi na kuvunja undugu)
Ndiyo inaweza kuangukia katika hayo na inaweza isiangukie...ndio maana nikakuambia kuwa ni suala linalotaka upambanuzi.
 
Naambiwa kuna masheikh huwa wanapangua itkaf. Eti mtu anashtakia kwa mungu halafu mungu akiachia adhabu yake - unakwenda kwa mganga anaipangua adhabu hiyo.

Unatoa hela kidogo tu - kuku /mbuzi nk.
 
Kikwete ni mwoga tu kwa sababu anjua maovu anayowafanyia watanzania ni mengi mno. Kwa vile sauti ya wengi ni sauti ya Mkuu wa nchi anaweweseka tu hajiamini.
 
Itikafu=ITIQAF.Neno hilo ni lakabu ya kiarabu. Itiqaf, ni ile hali ukaayo mahsusi kumuomba na kumlilia Mwenyezi Mungu juu ya yote yanayokusibu au kuomba msaada. Mara nyingi Itiqaf hufanyika katika zile siku 10 za mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani. Ambapo wachamungu wa kweli hukaa misikitini pasipo kujihusisha na masuala mengine yeyote ya kimaisha au kidunia wala kuongea na waaminio waingiao kusali zaidi ya 'Assalaam alaikhum' pekee. Kwamba waaminio wanaokaa Itiqaf basi muda wao wooote wa hizo siku 10 hutumika katika ibada tu, yaani kuongea na Mwenyezi Mungu tu. Mwisho huwa ni mwezi unapoandama na kuthibitishwa kuwa siku inayofuata ni Eid.JK amechanganya mambo, kuna kitu huitwa 'MUBAHALA'. Mubahala ndio hutumika rasmi kuamua NGUVU ya Muumba ichukue hatua. Tena Mubahala huwa ni wazi ambapo mshitaki na mshitakiwa wote hupeana taarifa rasmi (kubainisha muongo na mkweli), (apokelewaye dua na asiyepokelewa dua). Mubahala hutoa idadi ya siku maalum hukumu ya Muumba kuwa imetolewa.JK kachanganya kati ya 'itiqaf' na 'mubahala', anapaswa aingiliapo masuala ya dini awahusishe wanazuoni wa kiislam kumpatia tafsiri yenye tafsida nzuri kwa umma.Rock City.
1.Umejuaje kama kachanganya au wewe ni mmoja wapo wa waliomuombea afe?
2. Sasa hawa jamaa wanamuombea mtetezi na promoter wao afe tena?
Kuna jamaa hapa mtaani kwetu anasema hili neno limetokana na na neno itii cuf sasa inaonekana hii misikiti mi 3 inawanachama wengi wa cuf ndio maana wanamsomea hii dua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom