hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Itimar Ben Gvir
kichaa aliyepewa rungu,
Huyo ni mwanasiasa mtata na mwenyemsimamo mkali wa Israeli ambaye aliongoza harakati za kumpinga Netanyahu na kutaka ajiuzulu kwasababu ya kusitisha mapigano ya Gaza. Sasa Netanyahu amemchagua tena Itimar kuwa waziri wa usalama wa taifa wa Israeli.
Takwa la huyu jamaa toka mwanzo ni kuiweka Gaza chini ya Israeli daima. Sera zake za sasa ni kuiwekea Gaza vikwazo vikali na kuishambulia hadi pale ambapo wana Gaza wataamua kuachana na Hamas. Hivyo ukiona mashambulizi ya Gaza sasa jua yamesukumwa na Gvir na jopo lake la Wayahudi wenye msimamo mkali. Hivyo sasa ndio atakayekuwa anaongoza operation ya Gaza na wote ambao watachagua kupigana na Israeli.
Itimar pia ni mwanaharakati wa kuirejesha maeneo ya ufalme wa Yudea na Samaria ambao hata muda huu Wapalestina wanaondolewa katika maeneo hayo hasa katika ukingo wa magharibi wa mto wa Yordan ili kupisha ujenzi mpya wa makazi ya Wayahudi na upanuzi wa utawala wa Israeli kuu (greater Israeli).