Itoshe kusema CCM ni kisiki cha mpingo!

Itoshe kusema CCM ni kisiki cha mpingo!

Nchi ipo kwenye maandalizi Muhimu sana matatu kwa sasa,

1.maboresho daftari la kudumu la wapiga kura,

2.uchaguzi wa serikali za mtaa 2024

3.uchaguzi mkuu 2025...
Mambo yote haya yanahitaji muda wa kutosha, fedha za kutosha na umakini mkubwa.....
Unaweza kufanya marekebisho kwenye katiba mpya kitu ambacho kinawezakana kabisa
 
Kwa siasa za Tanzania ni CCM pekee inayoaminika kwa uhakika kwa wananchi kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, Sayansi na Techologia.

Ndio chama pekee chenye viongozi mahiri wa chama, zaidi sana ndicho chama pekee chenye uwezo wakusimamisha wagombea sahihi sana na makini mno nyakati za uchaguzi.

Ndio chama pekee chenye uwezo wa kisimamisha wagombea katika maeneo yote na vituo vyote vya kupiga kura nchini.

Ndicho chama chenye uwezo na uhakika wa kushinda uchaguzi wa Rais, ubunge,udiwani na serikali za mitaa kwa kishindo.

Ndicho chama pekee kinachoweza kufanya uchaguzi wa ndani na kubadili uongozi wa juu mpaka chini.

Ama kwa hakika, mbdala wa CCM kwenye siasa za Tanzania, hajazaliwa bado. Matumaini na Matarajio ya Maendeleo ya Watanzania ni kwa Chama Cha Mapinduzi.

Kidumu chama cha Mapinduzi.
nakukumbusha hujaandika namba ya simu mkuu
 
Unaweza kufanya marekebisho kwenye katiba mpya kitu ambacho kinawezakana kabisa
hakuna kinachowezekana kwa sasa kuhusu katba mpya ispokua hayo niliyo yaeleza hapo juu.

Ile kitu ndogo yawezafanyika ni kurekebisha sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi na kidogo tume ya uchaguzi
 
Sasa tume si iwe huru na huku mnakubalikana makada wa CCM wasiwe wasimamizi!
 
calm down Commander, ni mtazamo tu masela msijenge chuki

..DOLA inawabeba Ccm kwa kiwango kikubwa.

..pia Tanu / Ccm ilianzishwa miaka 38 kabla ya vyama vya upinzani kuanzishwa hapa Tanganyika / Tanzania.

..pamoja na kuzidiwa kiukwasi na kiumri ,vyama vya upinzani vimejipambanua na vimeizidi Ccm ktk kuwa na hoja zinazotetea wananchi.
 
Nchi ipo kwenye maandalizi Muhimu sana matatu kwa sasa,

1.maboresho daftari la kudumu la wapiga kura,

2.uchaguzi wa serikali za mtaa 2024

3.uchaguzi mkuu 2025...
Mambo yote haya yanahitaji muda wa kutosha, fedha za kutosha na umakini mkubwa.....

..matatizo ktk mfumo wetu wa uchaguzi yanajulikana kwa muda mrefu.

..tatizo ni kwamba kumekosekana utashi wa kuyatatua.

..Na utashi huo unakosekana kwasababu matatizo na kasoro ktk mifumo yetu ya uchaguzi ni moja ya turufu za ushindi za chama kilichoko madarakani.
 
Chama kinachokubalika hakiwezi kuwa kinaingiza kura zilizopigwa tayari kwa mgombea wake kwenye mabegi.

Chama kinachokubalika hakiwezi kuteka mawakala wa vyama pinzani.

Chama kinachokubalika hakiwezi kuwazimia mitandao ya kijamii kutoka October 28 hadi November 3.

Chama kinachofanya hivyo ni cha kijambazi na hakina uhalali wa kuongoza nchi.
images (36).jpeg
images (37).jpeg
images (38).jpeg
 
..matatizo ktk mfumo wetu wa uchaguzi yanajulikana kwa muda mrefu.

..tatizo ni kwamba kumekosekana utashi wa kuyatatua.

..Na utashi huo unakosekana kwasababu matatizo na kasoro ktk mifumo yetu ya uchaguzi ni moja ya turufu za ushindi za chama kilichoko madarakani.
mie nadhani utashi na nia ya serikali kushughulika na jambo hilo iko wazi kabisa na 2026 sio mbali hata kidogo.

Shida ni kukosekana kwa subra na ustahimilivu kwa miongoni mwa makundi binafsi ya wasioridhika na wenye tamaa za vyeo na madaraka ya kisiasa....
 
Chama kinachokubalika hakiwezi kuwa kinaingiza kura zilizopigwa tayari kwa mgombea wake kwenye mabegi.

Chama kinachokubalika hakiwezi kuteka mawakala wa vyama pinzani.

Chama kinachokubalika hakiwezi kuwazimia mitandao ya kijamii kutoka October 28 hadi November 3.

Chama kinachofanya hivyo ni cha kijambazi na hakina uhalali wa kuongoza nchi.
View attachment 2814564View attachment 2814565View attachment 2814566
hili igizo halijawahi kuthibitika na kuleta badiliko lolotsee....

Tuliahidi, tumetekeleza, tunasonga mbele....
 
..DOLA inawabeba Ccm kwa kiwango kikubwa.

..pia Tanu / Ccm ilianzishwa miaka 38 kabla ya vyama vya upinzani kuanzishwa hapa Tanganyika / Tanzania.

..pamoja na kuzidiwa kiukwasi na kiumri ,vyama vya upinzani vimejipambanua na vimeizidi Ccm ktk kuwa na hoja zinazotetea wananchi.
Wananchi gani hao?, unamaanisha Yanga right?
 
mie nadhani utashi na nia ya serikali kushughulika na jambo hilo iko wazi kabisa na 2026 sio mbali hata kidogo.

Shida ni kukosekana kwa subra na ustahimilivu kwa miongoni mwa makundi binafsi ya wasioridhika na wenye tamaa za vyeo na madaraka ya kisiasa....

..naheshimu maoni yako.

..Ccm haikutekeleza kwa kikamilifu mapendekezo ya tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali kuhusu namna ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

..Ripoti ya Jaji Nyalali ilitoka mwaka 1992 au 1993. Huwezi kusema Watanzania hawana subira au ustahamilivu wakati wamekuwa waungwana na wamevumilia hali iliyopo kwa miaka 30+.
 
Kwa siasa za Tanzania ni CCM pekee inayoaminika kwa uhakika kwa wananchi kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, Sayansi na Techologia.

Ndio chama pekee chenye viongozi mahiri wa chama, zaidi sana ndicho chama pekee chenye uwezo wakusimamisha wagombea sahihi sana na makini mno nyakati za uchaguzi.

Ndio chama pekee chenye uwezo wa kisimamisha wagombea katika maeneo yote na vituo vyote vya kupiga kura nchini.

Ndicho chama chenye uwezo na uhakika wa kushinda uchaguzi wa Rais, ubunge,udiwani na serikali za mitaa kwa kishindo.

Ndicho chama pekee kinachoweza kufanya uchaguzi wa ndani na kubadili uongozi wa juu mpaka chini.

Ama kwa hakika, mbdala wa CCM kwenye siasa za Tanzania, hajazaliwa bado. Matumaini na Matarajio ya Maendeleo ya Watanzania ni kwa Chama Cha Mapinduzi.

Kidumu chama cha Mapinduzi.
NONSENSE!!!!!
 
Hivi mtu mzima kujikomba inaleta tafsiri gani?
inaleta tafsiri ya kutamani kujifunza na kuongeza uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini na duniani kisiasa, kiuchumi na kijamii....

ikiwa huna haja ya hayo unatulia tuli na kupita kimyakimya haidhuru....

Hata hivyo, hongera kutumia uhuru wako wa kutoa maoni 🐒
 
..naheshimu maoni yako.

..Ccm haikutekeleza kwa kikamilifu mapendekezo ya tume ya Jaji Mkuu Francis Nyalali kuhusu namna ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

..Ripoti ya Jaji Nyalali ilitoka mwaka 1992 au 1993. Huwezi kusema Watanzania hawana subira au ustahamilivu wakati wamekuwa waungwana na wamevumilia hali iliyopo kwa miaka 30+.
nikuhakikishie under Dr SSH administration, 2026 tunapata katiba mpya na madhaifu yote ya nyuma yatazikwa rasmi kwenye katiba mpya kama hiyo ndio muarobaini wa changamoto zote nchini....

Let's relax, wait and see it
 
Back
Top Bottom