ITrust Finance yazindua mfuko wa iDollar kwa Uwekezaji kwa Dola ya Marekani,

ITrust Finance yazindua mfuko wa iDollar kwa Uwekezaji kwa Dola ya Marekani,

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
WhatsApp Image 2025-07-10 at 22.32.57_024fc13f.jpg

Kampuni ya ITrust Finance imezindua rasmi Mfuko wa IDollar, mfuko wa pamoja wa soko la fedha unaotumia sarafu ya Dola ya Marekani (USD)

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Julai 10, 2025 ambapo kampuni hiyo imeeleza kiwa mfuko huo umezinduliwa kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania kulinda na kukuza mali zao kupitia njia salama, rahisi na yenye tija.

Imeelezwa kuwa Mfuko wa iDollar unatoa nafasi kwa watu binafsi na taasisi kuwekeza kwenye dhamana na hati fungani za muda mfupi hadi wa kati kwa kutumia Dola ya Marekani. Kampuni hiyo imeeleza kuwa mfuko huu unaleta mapato ya ushindani ikilinganishwa na amana za kawaida za benki, huku ukitoa faida ya upatikanaji wa fedha kwa urahisi, usimamizi wa kitaalamu, pamoja na kinga dhidi ya kuporomoka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania.
WhatsApp Image 2025-07-10 at 22.32.54_d6c82192.jpg

WhatsApp Image 2025-07-10 at 22.33.00_e7f87a2f.jpg

Aidha imeelezwa kuwa kuanza kuwekeza, mwekezaji anatakiwa kuwa na angalau Dola 1,000 za Marekani, huku kiwango cha chini cha nyongeza ya uwekezaji kikiwa ni Dola 100. Wawekezaji wanatakiwa kushikilia uwekezaji wao kwa kipindi cha siku 90 kabla ya kuweza kutoa fedha, ingawa hakuna ada yoyote ya kujitoa.

Mfuko wa iDollar umetengenezwa mahsusi kwa watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi zinazotafuta njia salama, thabiti na yenye mapato ya uhakika ya uwekezaji.

Faida nyingine za mfuko kuhusu mfuko huo, ni pamoja na mapato ya juu kuliko amana za benki kwa sarafu ya dola, uwezo wa kutoa fedha kwa urahisi baada ya kipindi kifupi, mseto wa uwekezaji unaosaidia kupunguza hatari, na uwazi kupitia ripoti ya kila siku kuhusu mwenendo wa mfuko.

Vilevile, imeelezwa kwamba mapato yatokanayo na mfuko huu hayatozwi kodi kwa mujibu wa sheria za Tanzania, huku usalama wa mali za wawekezaji ukidhibitiwa na Benki ya CRDB kwa usimamizi wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Mchakato wa kujiunga na mfuko huu unaanza kwa kufungua akaunti kupitia tovuti ya Trust Finance, ambapo mwekezaji atapokea barua pepe ya ukaribisho pamoja na kitambulisho cha mteja na maelezo ya akaunti ya mfuko. Baada ya kuweka fedha na kutuma uthibitisho wa malipo, mwekezaji hupokea risiti rasmi ya uwekezaji wake.

Profesa Mohammed Warsame, mmoja wa Wakurugenzi wa iTrust Finance Limited, alisema kuwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kutoa miongozo mipya inayozuia matumizi ya dola ndani ya nchi katika baadhi ya miamala, wameona umuhimu wa kuanzisha mfuko huu unaotoa nafasi kwa watu kuwekeza kwa dola bila kuvunja sheria. Alibainisha kuwa fedha za wawekezaji zitawekwa na kurejeshwa kwa mfumo ule ule wa Dola.
WhatsApp Image 2025-07-10 at 22.32.58_bd8f447d.jpg

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, CPA Nicodemus Mkama, alisema kuwa mfuko huu ni hatua kubwa katika historia ya sekta ya fedha nchini. Alieleza kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania inapata mfuko wa pamoja unaowezesha uwekezaji wa moja kwa moja kwa fedha za kigeni. Alisisitiza kuwa mafanikio haya yametokana na jitihada za Serikali katika kuweka sera na sheria wezeshi kwa mazingira bora ya uwekezaji.

ITrust Finance Limited ni kampuni ya huduma za kifedha inayosajiliwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania na CMSA, ikiwa na hadhi ya kuwa mkopeshaji wa Daraja la Pili. Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2013 na hutoa huduma kwa watu binafsi, biashara na taasisi mbalimbali.
 
Ina oparate kama utt amis kwamba Kuna gawio la mwezi? Au ndo unasubili rate ya dollars
 
Back
Top Bottom