Hayawi hayawi, yamekuwa! Hatimaye Mh Edward Ngoyai Moringe Lowassa amepata fursa ya kutembea nchi nzima kuwashukuru wananchi waliompigia kura kwa kishindo na kupelekea UKAWA kuongeza idadi ya wabunge kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na chama chochote cha upinzani tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CHADEMA na aliyekuwa mgombea nafasi ya urais kwa mwavuli wa UKAWA, atafanya mikutano nchi nzima kwa lengo la kukijenga chama na kuwashukuru wananchi waliompigia kura na watakaompigia kura katika uchaguzi mkuu wa 2020.
Chanzo: Mwananchi
MAONI YANGU
Nampongeza baba Lowassa kwa juhudi zake za kukijenga chama na kufanya maandalizi ya uchaguzi ujao mapema. Wakati CCM wanatoana ngeo kugombania nafasi ya ukatibu mkuu wa chama, UKAWA wanajipanga kuichukua nchi 2020. Hizi mbinu za kisayansi ni muhimu sana na zitafanikisha ushindi wa kishindo kwa UKAWA mnamo mwaka 2020. Viva Lowassa, Viva UKAWA.
Bila kupigania mabadiliko ya katiba, hakuna kitu kiongozi. Upinzani hauhitaji nguvu kubwa kupata kura za kutosha. Nguvu kubwa zipelekwe kwenye kudai katiba mpya ambayo ndiyo suluhisho la kutangazwa kwa mshindi!. Kwa nini tuzungeke mbuyu?
Kama hatutakuwa na mpango madhubuti wa kupatikana katiba ya wananchi, ninaomba hizo fedha za mkutano, zinunue sukari, Isambazwe nchi nzima wauziwe wanachama wa UKAWA waliopo na wanaojiunga. Tena kwa sababu ya sukari na maisha kuzidi kuwa magumu huku kina Lugumi wakilindwa kwa nguvu zote za serikali ya ccm, wanachi kutelekezwa wakifa kwakukosa huduma za afya huku waliojidai kwamba watawapa mabadiliko wakionyesha hata hawayajui mabadiliko yaliyokuwa yanaletwa na UKAWA, na kwamba hata nia wala maono na uwezo wa mabadiliko hawana zaidi ya sarakasi za kisanii, UKAWA watengenze kadi nyingi sana za wanachama wapya. Wazitawanye nchi nzima, na sukari kwa wingi ili wanachama wao wnaunue.
Wabaki CCm wakipiga makofi pamoja na miayo! Duh, aibu hiii!!!!!!!!!!1