The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Hali ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani imefikia kiwango cha kutisha sana, majuzi hapa nilikuwa nasafiri na gari majira ya usiku wa manane, askari akanisimamisha nikakutwa na makosa, nikamwomba anisamehe akakataa kunisamehe, nikamwambia basi naomba uniandikie faini, akafoka kwa sauti "nikikuandikia faini mimi nitapata nini?". Mara akatoa pingu akanifunga mikono akanipeleka kwenye defender la polis.
Nikiwa ndani ya hilo defender akaja askari wa cheo kidogo akaniambia we unakumbali usumbufu wa kwenda kulala mahabusu kuliko kutuachia hata elfu 5!?
Nikawambia elfu 5 sina wakaniambia ubahili wako utakusababishia hasara kubwa nilipoona hivyo ikabidi niwape shs 2000 wakanifungua pingu huku wanacheka.
Kitendo kile kiliniuma sana. Ndipo nikapata hoja, hivi haiwezekani itungwe sheria kuhalalisha hii rushwa ili angalau basi iwe rasmi.
Maana nahisi kuizuia haiwezekani.