Hope urassa
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 4,230
- 10,650
Asante kusikia hivyo..Poa kabisa mom
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kusikia hivyo..Poa kabisa mom
Amina….vp midnight mmeachiwa huru?Asante kusikia hivyo..
Ngoja nkachekiAmina….vp midnight mmeachiwa huru?
🤣🤣🤣moto mnao…. Vincenzo Jr kawaponza aiseeNgoja nkacheki
Kongole sana ndugu Mmanyanigho kwa ujasiri wako wa kutetea haki ya binadamu mwenzako dhidi ya uonevu wa "majambazi katika sare".Umenikumbusha tukio nililoshuhudia siku chache nyuma kati ya dereva, konda na abiria wa daladala(mimi nikiwemo) na trafiki.
Mimi nilipandia gari barakuda, ilikua inaenda manzese (chang'ombe to kg/mburahati).
Tumefika vingunguti kona, askari akasimamisha akimtuhumu dereva kuchora(kageuzia njiani, yaani hajafika chang'ombe).
Likazuka zogo la kufa mtu pale, dereva hakubali, zogo likahamia ndani ya gari askari alipochomoa funguo ya gari. Abiri wote tulikua upande wa dereva na kuahidi kutoa full support ikihitajika...
Askari kuona vile akaamuru gari iende kituoni kwa maelezo zaidi, na pia akatoa kama kitisho hivi, kua kama abiria una haraka shuka kapande gari nyingine uendelee na ishu zako, kama unataka kwenda kutoa ushahidi basi baki ndani ya gari twende wote kituoni(buguruni).
Wakashuka baadhi tukabaki abiria kama 12 hivi. Gari ikawashwa tukaenda mpaka buguruni, kabla ya kuingia kituoni yule askari akarudia kuusema "kama una shughuli zako, kituo kile pale nenda kapande gari uendelee na harakati zako, kama upo pamoja na huyu dereva basi twende ukatoe ushahidi".
Kitisho kikafika wakashuka tena wachache wakasepa, gari ikaingizwa ndani ya kituo cha polisi.
Mpaka hapo tumebaki kama 7 hivi, tukaingia ndani ya kituo, dereva akaingizwa ndani ya counter kule akachuchumaishwa chini.
Yule askari akatoa maelezo kwa mkuu wa kituo akimkandia vilivyo dereva wetu(ila polisi hawa aisee).
Akarudi kwetu tena, akasema kwa karipio kwa koplo kua aandike taarifa zetu ili tukamtetee mahakamani yule dereva. Sote tulikua tayari kuandika taarifa zetu pia.
Mkuu wa kituo ikabidi aingilie kati baada ya kuona sisi bado tuko na dereva kua hajageuza gari bali pale kati yetu wapo waliopandia gari mwisho na tupo tuliona gari ikienda na kurudi barakuda tukapanda, na wapo walioenda kugeuza na gari kabisa.
Mkuu wa kituo, alikua mnyenyekevu tofauti na yule askari wake, alitupa risala kidogo pale na akamuamuru konda arudishe nauli zetu, lahaulah akaambiwa hata nauli hatokutoa bado. Mshangao wa wazi ulionekana usoni mwake maana alidhani tupo pale kisa konda ana nauli zetu kumbe wala hata nauli hatukulipa ni tumeenda kumtetea dereva tu.
Akatutoa hofu pale na brah brah za kutushusha mori pale na kuahidi yule bwana(dereva) yuko salama na haki yake itapatikana sisi tuendelee na shughuli zetu.
Basi tukabadilishana mawasiliano na konda pale, tukawaacha sisi haoo tukasepa zetu.
Yule askari alitaka rushwa toka kwa dereva, ila dereva hakua tayari kutoa. Na yule askari sijamuona tena njia ya huku sijui kahamishiwa wapi yule bwana.
Naskiaga wakizingua wanapelekwa sehemu zisizo na maokoto.
Wamegeuka wakusanya mapatoNi askari wachache pekee wa usalama barabarani ndiyo hawaendekezi vitendo vya rushwa. Ila walio wengi, nadhani wanaendekeza sana rushwa.
Mimi nashauri ziwekwe camera za cctv barabarani ili kurekodi matukio ya uvunjaji wa sheria kwa madereva. Na kwa upande wa askari, wabakizwe wachache tu kwenye check points.
Kiukweli askari wa usalama wamekuwa ni wengi barabarani mpaka wamegeuka kuwa keto kwa madereva. Kila baada ya kilomita moja, unasimamishwa na kuulizwa vitu vile vile! Na kama siyo hivyo, basi utakuta dereva unawindwa na tochi kwenye vibao vya 50 KMH ili tu utafutiwe kosa la kutoa rushwa!
This is too much.
Wakuhalalisha traffic watakausha watu walai
Yaani wangekuwa wanakusanya inaingia serikalini isingekuwa neno sasa ni zao za mfukoni huku mshahara na posho wanapiga kama kawaWamegeuka wakusanya mapato
Hivi ni ccm pekee kuna rushwa au hata vyama vingne ipo?CCM imeshindwa kabisa kudhibiti Rushwa kwa sababu ndani ya chama chaguzi zote bila RUSHWA hupiti baya zaidi Uchaguzi wa 2020 tumeshuhudiwa Nchi ikiwa na WABUNGE wasio na Chama ndani ya Bunge letu kwani Upatikanaji wao ni Siri yao CCM na Tume ya Uchaguzi
Hali ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani imefikia kiwango cha kutisha sana, majuzi hapa nilikuwa nasafiri na gari majira ya usiku wa manane, askari akanisimamisha nikakutwa na makosa, nikamwomba anisamehe akakataa kunisamehe, nikamwambia basi naomba uniandikie faini, akafoka kwa sauti "nikikuandikia faini mimi nitapata nini?". Mara akatoa pingu akanifunga mikono akanipeleka kwenye defender la polis.
Nikiwa ndani ya hilo defender akaja askari wa cheo kidogo akaniambia we unakumbali usumbufu wa kwenda kulala mahabusu kuliko kutuachia hata elfu 5!?
Nikawambia elfu 5 sina wakaniambia ubahili wako utakusababishia hasara kubwa nilipoona hivyo ikabidi niwape shs 2000 wakanifungua pingu huku wanacheka.
Kitendo kile kiliniuma sana. Ndipo nikapata hoja, hivi haiwezekani itungwe sheria kuhalalisha hii rushwa ili angalau basi iwe rasmi.
Maana nahisi kuizuia haiwezekani.
Big up Hilo la kuvaa kamera ni tiba ila hadi tufike huko!!......Waongezewe mishahara pamoja na maslahi yao kuboreshwa. Iwe sheria askari wa barabarani kuvaa camera.
😂😂🤣🤣🤣moto mnao…. Vincenzo Jr kawaponza aisee
Nakerwa sana na hawa viumbe barabarani,hasa wa barabara ya Morogoro, eneo kati ya kibaha na mlandizi wanavyonikera hadi nimewapa jina la kunguru weupe kwani hamna uchafu unaokatiza mbele yao salama.Ila kwangu wanaambulia manyoya tu tena bila kupoteza muda,maneno mawili tu,andika faini.Hali ya rushwa kwa askari wa usalama barabarani imefikia kiwango cha kutisha sana, majuzi hapa nilikuwa nasafiri na gari majira ya usiku wa manane, askari akanisimamisha nikakutwa na makosa, nikamwomba anisamehe akakataa kunisamehe, nikamwambia basi naomba uniandikie faini, akafoka kwa sauti "nikikuandikia faini mimi nitapata nini?". Mara akatoa pingu akanifunga mikono akanipeleka kwenye defender la polis.