Itungwe sheria kuhalalisha rushwa ya trafiki ili walau tuambulie kodi

Kongole sana ndugu Mmanyanigho kwa ujasiri wako wa kutetea haki ya binadamu mwenzako dhidi ya uonevu wa "majambazi katika sare".
MUNGU akubariki sana ndugu.
 
Wamegeuka wakusanya mapato
 
Hivi ni ccm pekee kuna rushwa au hata vyama vingne ipo?
 
Ukifatilia ni kweli akuandikie faini ya 30k ikaliwe na mawaziri au wabunge au umpe buku 5 akale yeye na familia yake mgawane umaskini
 

Waongezewe mishahara pamoja na maslahi yao kuboreshwa. Iwe sheria askari wa barabarani kuvaa camera.
 
sasa una makosa ka aftano nako huna sasa usaidiweje.....
alafu kosa gani hilo mpka pingu mbona mambo ya barabarani tunamaliza bila hata kushikana wala mapingu au ulikua na magendo nn🤣
 
Nakerwa sana na hawa viumbe barabarani,hasa wa barabara ya Morogoro, eneo kati ya kibaha na mlandizi wanavyonikera hadi nimewapa jina la kunguru weupe kwani hamna uchafu unaokatiza mbele yao salama.Ila kwangu wanaambulia manyoya tu tena bila kupoteza muda,maneno mawili tu,andika faini.
 
Chagua Chadema maana ujinga kama huu wa rushwa kwa hawa polisi wetu utadhibitiwa ipasavyo. Ccm imewashindwa Maana Kwa ccm rushwa ni kawaida sana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…