Itungwe sheria ya kufuatilia na kudhibiti mapato na matumizi katika Nyumba za Ibada

Wotu tunafahamu kuwa serikali haina dini ila ni serikali hii hii inayosimamia uanzishwaji wa makanisa na misikiti na hata kuyasajili.

Binafsi naona wakati umefika serikali isiishie katika kuyasajali tu makanisa haya bali tuwe na sheria itakayoruhusu serikali kupitia chombo/maafisa maalumu kukagua matumizi na mapato katika nyumba za ibada.

Nasema hivi kwassababu siku hizi katika makanisa yetu(sisi wakristo) tumekuwa na michanga mingi kwa jina la sadaka,n.k mpaka inakuwa kero kwa waumini.

Hoja yangu ni kuwa,japo kunaweza kuwa na udhibiti ndani ya nyumba zetu hizi za ibda,lakini nadhani kuna umuhimu wa kuwa na udhibiti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha hizi utakaokuwa unafanywa na chombo kutoka serikalini kama extenal auditer.

Vile vile sheria hiyo itumike katika kusimamia aina ya michango inayoanzishwa kuanzia katika ngazi za jumuiya mpaka makanisani na ikiwezekana kuwe na ukomo wa kiwango cha kuchangisha waumini na kama itabidi kuvuka kikomo kilichowekwa, basi kanisa husika lipaswe kuomba kibali au kutoa taarif kwa chombo kitakachoanzishwa na ambacho kitakauwa mamlaka ya kudhibiti mapato na matumizi katika nyumba zetu za ibada.

Na ili kuondoa uwezekano wa kutokea mgongano au mgogoro baina ya serikali na taasisi za kidini,chombo hichi kiundwe kwa kushirikisha serikali na taasisi zote za dini.

Tusisahau kuwa baadhi ya viongozi katika siasa au vyama vya siasa,taasisi za serikali,taasisi binafsin.k ndio wakati mwingine huwa ni viongozi katika taasisi hizi za kidini hivyo kama wanakaguliwa katika taasisi zingine wanazoziongoza,basi hata katika taasisi hizi za kidini pia wakaguliwe jinsi wanavyodhibiti na kusimamia mapato na matumizi katika nyumba za Ibada.

Kama tunavyoona umuhimu kuwa na sheria ya kudhibiti mapato na matumizi katika vyama vya siasa,vyama vya ushirika,SACCOS,n.k,umuhimu huo pia unahitajika katika nyumba zetu za ibada kwani siku hizi mambo katika nyumba zetu za ibada yamebadilika sana tofauti na siku za nyuma.

Ni kweli serikali haina dini,lakini waumini katika taasisi hizi za kidini ndio hao hao ambao wanaunda SACCOS,vyama vya ushirika,n.k ambako serikali ina mkono wake katika uendeshaji wa taasisi hizi ili kulinda masilahi ya wananchi wake.

kwa mwaka unatoa michango ya kiasi gani.!?

kati ya sadaka,majitoleo,shukrani,zaka,bahasha maalum na mengineyo...kama ulivyoonyesha!?

na pia hujaeleza hiyo michango unalazimishwa ama unatakikana utoe kwa hiari kadiri Mungu alivyokujalia
 
Kutoa sadaka sio lazima ni hatari. Mumi ni Mkristi, sijawahi kulazimishwa kutoa sadaka, natoa kadiri Arogo anavyoniongoza

Ukiona unaposali sadaka zake hauziwezi, nenda kanisa lingine ambali halina sadaka nyingi au hawatoi sadaka.

Au unaweza ukakaa bila dini, haulazinishwi.

Ila usiwalazimishe watu wengine walioamua kwa hiyari yao na kwa imani yao wanaona inafaa kutoa hizo sadaka na michangi, eti watungiwe sheria ya kuweka kiwango. Hiyo serikali inamjua Mungu hadi iweke kiwango?

Hebu kajifunze kwanza kuandika kwa usahihi kisha urejee kuchangia hapa ,sababu inavyo onekana hata kilicho andikwa haukukielewa kabisa.
 
kwa mwaka unatoa michango ya kiasi gani.!?

kati ya sadaka,majitoleo,shukrani,zaka,bahasha maalum na mengineyo...kama ulivyoonyesha!?

na pia hujaeleza hiyo michango unalazimishwa ama unatakikana utoe kwa hiari kadiri Mungu alivyokujalia

Mkuu Imani zimegeuka kuwa ni Biashara na sio suala la kiroho ,utakapo hitaji Huduma kama kubatiza Mtoto utakutana na msufuru wa Sadaka na Majina yake unakusubiri ufanye hivyo ndio Mwanao abatizwe.

Nimewahi kuwaachia fomu zao kwa Sababu hizo hizo ,hii ina maana ukiwa Masikini kupata Huduma sahihi na kwa wakati ni ngumu mno.
 
Mleta mada sasa unataka serikali iingilie kila mahali .Kwa dini zote hamna hata moja ambayo inalazimisha kutoa michango au sadaka ila kwa kuwa unahali mbaya kimaisha na ulizoea kutoa hiyo michango lkn kwa kuwa sasa unaona kabisa huwezi unaona ni bora serikali iingilie kati.
Kwangu mimi nasema siyo sahihi kabisa na serikali ikijaribu italeta mgongano mkubwa sana wa serikali na dini na hiyo vita yake siyoi mashara mfano tunao kule Nigeria.

Tatizo lipo wapi?
Maisha yamekuwa magumu na yanaendelea kuwa magumu kwa awamu hii ya tano chini ya CCM

Nini kifanyike?
1. Serikali ibadili kama siyo kuacha mfumo huu wa tumbuatumbua maana haijaleta mafanikio kabisa,huko kwenye halmashauri bado miradi inaendelea kukwama kutokana na uzembe au ufisadi kila inapoitwa siku mpya mfano Safari zote za Mh Waziri mkuu na hata za Rais mwenyewe wa nchi Dr.John Pombe Magufuli
2.Serikali ifuate katiba ktk kuongoza mfano mishahara ya watumishi wa umma inatakiwa kuongezwa kila mwaka (annual increment) lakini huu ni mwaka wa nne haijaongeza

Mishahara ikiongezwa na madeni yakilipwa inavyostahili , vijana waliomaliza vyuo kwenye kada mbali mbali kuajiriwa (mfano kada ya ualimu wapo wengi mtaani lkn kuna baadhi ya shule hamna walimu)then maisha yatarudi sehemu yake na hutaona popote watu wanalalamika kuhusu michango sijui ya harusi,sijui nimemzomesha GF na etc
 
Wotu tunafahamu kuwa serikali haina dini ila ni serikali hii hii inayosimamia uanzishwaji wa makanisa na misikiti na hata kuyasajili.

Binafsi naona wakati umefika serikali isiishie katika kuyasajali tu makanisa haya bali tuwe na sheria itakayoruhusu serikali kupitia chombo/maafisa maalumu kukagua matumizi na mapato katika nyumba za ibada.

Nasema hivi kwassababu siku hizi katika makanisa yetu(sisi wakristo) tumekuwa na michanga mingi kwa jina la sadaka,n.k mpaka inakuwa kero kwa waumini.

Hoja yangu ni kuwa,japo kunaweza kuwa na udhibiti ndani ya nyumba zetu hizi za ibda,lakini nadhani kuna umuhimu wa kuwa na udhibiti na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha hizi utakaokuwa unafanywa na chombo kutoka serikalini kama extenal auditer.

Vile vile sheria hiyo itumike katika kusimamia aina ya michango inayoanzishwa kuanzia katika ngazi za jumuiya mpaka makanisani na ikiwezekana kuwe na ukomo wa kiwango cha kuchangisha waumini na kama itabidi kuvuka kikomo kilichowekwa, basi kanisa husika lipaswe kuomba kibali au kutoa taarif kwa chombo kitakachoanzishwa na ambacho kitakauwa mamlaka ya kudhibiti mapato na matumizi katika nyumba zetu za ibada.

Lengo la kuwa na ukomo katika michango hii ni ili kuzuia waumini wasio na uwezo kukamuliwa michango isioendana na vipato vyao halisi na pia kudhibiti michango inayoweza kuwa na ulakini lakini kwa alie tayari kuchagia zaidi, aruhusiwe mradi tu muhusika mwenyewe ameridhia.

Na ili kuondoa uwezekano wa kutokea mgongano au mgogoro baina ya serikali na taasisi za kidini,chombo hichi kiundwe kwa kushirikisha serikali na taasisi zote za dini.

Tusisahau kuwa baadhi ya viongozi katika siasa au vyama vya siasa,taasisi za serikali,taasisi binafsin.k ndio wakati mwingine huwa ni viongozi katika taasisi hizi za kidini hivyo kama wanakaguliwa katika taasisi zingine wanazoziongoza,basi hata katika taasisi hizi za kidini pia wakaguliwe jinsi wanavyodhibiti na kusimamia mapato na matumizi katika nyumba za Ibada.

Kama tunavyoona umuhimu kuwa na sheria ya kudhibiti mapato na matumizi katika vyama vya siasa,vyama vya ushirika,SACCOS,n.k,umuhimu huo pia unahitajika katika nyumba zetu za ibada kwani siku hizi mambo katika nyumba zetu za ibada yamebadilika sana tofauti na siku za nyuma.

Ni kweli serikali haina dini,lakini waumini katika taasisi hizi za kidini ndio hao hao ambao wanaunda SACCOS,vyama vya ushirika,n.k ambako serikali ina mkono wake katika uendeshaji wa taasisi hizi ili kulinda masilahi ya wananchi wake.
Upo sawa 100%
 
Attachments

  • VID-20191023-WA0003.mp4
    4.7 MB
  • VID_22930201_200846_985.mp4
    5.6 MB
  • VID_22880815_015307_168.mp4
    4.9 MB
  • VID_22930201_200846_985.mp4
    5.6 MB
Nikweli hesabu za Manisa zipitiwe kuondo utapeli kwa kulitumia jina la bwana!!
Kuna baadhi ya manabii wanauza maji,mafuta,picha zao,chumvi,vitabu,upako na wanapiga super profit lkn kodi hawalipi hili halikubaliki wao wanaishi kifahari waumini wao hawajui walenini
 
Back
Top Bottom