Sheria zilizopo hazijatosha kutupelekea tuwe na maudhui ya msingi yenye kulenga kutoa priority kwenye maadili,uchumi,elimu na maendeleo inapokuja swala la matumizi ya vyombo vya habari na teknolojia za mawasiliano.
Lazima kama Taifa tuwe na mtaala wa maudhui ya habari na comments katika mitandao.
Ni muhimu kuwa na miongozo ya nini kichangiwe (kijadiliwe) na kwa kiasi gani .
mfano kila media lazima iwe na Taarifa zinazohusu Siasa safi,maswala ya afya,elimu ya uchumi,historia bora ya Tanzania,kilimo,sayansi,hesabu,ustawi wa jamii ,michezo ,n.k
sio hii shakara baghara tunayoiona sasa
Unaliangalia tatizo kutoka upande mbaya.
Umekuwa kama mtu mwenye nyundo, ambaye anataka kutatua kila tatizo kwa kutumia nyundo, hata nzi akitua kwenye kidole chake, badala ya kumfukuza tu, atataka kukipiga hicho kidole nyundo amuue yule nzi. Mwishowe atajiumiza kidole mwenyewe.
Sheria ndiyo nyundo hapo.
Wewe ni kama mtu ambaye hataki mguu wake ukanyage ardhi, halafu ana uchaguzi kati ya mambo mawili, ama avae kiatu, ama atandaze zulia (carpet) dunia nzima ili asikanyage chini, wewe unachagua kutandaza zulia dunia nzima badala ya kuvaa kiatu tu.
Tanzania kuna kasumba ya kufikiri sheria itataua kila tatizo.
Wakati kuna matatizo ya elimu, kuna tatizo la utamaduni, kuna matatizo ya siasa, kuna tatizo sasa hivi nchi inazalisha wajinga masikini wengi, ambao na wao wakifika miaka 18 mpaka 20 tu, wanazalisha masikini wajinga wengine.
Kuna tatizo la umasikini. Mtu mwenye njaa unaweza kumuwekea sheria na asiiogope, kwa sababu ataona bora achukue chance ya kufungwa kuliko kufa kwa njaa. Ndiyo maana umalaya umepigwa marufuku kisheria, watu wanakamatwa, lakini hawaachi.
Tanzania ina watu takriban milioni 72, na inaongeza watu milioni 2 kila mwaka.
Marekani ina watu milioni 342, zaidi ya mara nne ya Tanzania, lakini inaongeza watu milioni 1.8 tu kila mwaka. Na hapo kwa Marekani kuna wahamiaji kibao.
Mpaka hapo hujaona tuna tatizo la zaidi ya sheria tu?
Hii population bomb ya 2.8 -3% yearly increase inayopelekea idadi ya watu kufikia milioni 140 by 2050, huimalizi kwa kutunga sheria tu. Hili ni jambo litakaloenda na utamaduni na elimu.
Tanzania kuna mikoa ambayo, hususan kwa wanawake, literacy rates zipo around 75%. Maana yake, katika kila watu wanne, mmoja hajui kusoma na kuandika hapo. Na hizo ni takwimu rasmi za seeikali ambazo zimechakachuliwa, maana yake uhalisia ni mbaya zaidi.
Hao ni wanaojua kusoma na kuandika kwa viwango vya serikali tu, ukizidisha viwango unaweza kukuta nusu ya Watanzania hawajui kusoma, kuandika, kwa ufahamu na mantiki na kidhahania.
Hilo janga hulimalizi kwa sheria ya kuwachunga watu mtandaoni kama ng'ombe.
Watu wajinga hata hiyo sheria yako hawataijua, na wakiijua hawataijali. Na watakushinda kwa wingi wao tu.
Watu wanaopost mambo bila maadili mitandaoni hawaogopi sheria, na hakuna jeshi la kulinda maadili litakalotosha kuwaweza hawa watu bila ya kuvunja haki za wengine mitandaoni.
Na kabla huja address mambo ya utamaduni, mambo ya elimu, mambo ya ajira, mambo ya uchumi, baada ya miaka michache yatatokea mambo ambayo utatamani haya ya sasa yarejee. Kutakuwa na mitandao ya video za ngono za wazi za Kitanzania mpaka utashangaa mwenyewe. Sasa hivi mitandao ipo, lakini hii ya sasa ni kama wanajaribu tu, itakayokuja baada ya miaka mitano tu, itakuwa hatari mara nyingi sana kuzidi ya sasa.
Ukibisha rejea hapa niaka mitano ijayo.
Haya ni mambo ambayo huwezi kuyamaliza kwa sheria, ni matatizo ambayo hayajaanza siku moja, si tatizo moja ni mambo mengi sana ya mmomonyoko wa maadiki katika jamii yametufikisha hapa, hivyo, utatuzi wake hauwezi kuwa sheria ya mara moja.
Tatizo mnatazama tunapoangukia, hamtazami tulipojikwaa.
Ukiona tatizo linajitokeza leo kwa vijana, usiangalie hao vijana, anza na wazazi wao wamezaliwa lini, wamelelewa vipi, kuna matatizo gani katika jamii yetu kwenye miaka angalau 30 iliyopita?
Ukiangalia hapa tulipo tu, ulete sheria gani kupiga mafufuku hiki na kile ushafeli tayari.