ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Uzi mzuri...
 
Nafikiri kila mkoa waliwekewa li-itv likubwa uwanjani tulikua tunaenda kuangalia tausi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Shyrose Bhanjia alikuwa TBC kama sikosei
Mkuu kulikuwa na kibinti fulani kilikuwa shombe ITV kilikiwa sijui kinamalizia mimi ni sharifa tatadoo wa ITV hata sijui kama nimepatia jina, unakikumbuka.
Basi enzi hizo sisi tulikuwa tunadhani kila mtoto mzuri anayetokea kwenye tangazo ni mtoto wa mengi.
Kulikuwa na tangazo la revora soap.
Demu anaoga kwenye jacuz, anaambiwa tueleze siri ya mafanikio yako, anajibu sio siri ni revora. Sijui anaendelea kwani moisture yake ni tulivu na huniweka fresh mchana kutwa.
Nilikuwa nadhani mtoto wa mengi na nilikuwa kid ila namwelewa kinoma
 
Daaah unanikumbusha those days ninakula ugali wa baba na mama sikua na stress za sijui kodi, sijui bili za maji umeme,kabisa kucheki hizo comedy familiy matters, bill cosby, robocop, na nyingine nyingi, baada ya hapo naingia bed kulala huku nikila ngoma tamu kwenye redio mzee alinipa either ni flash backs, bongo fleva, R&B toka Redio free Africa huku kwa nje kuna Kamvua Mvua mwanana kananisindikiza usingizi wangu!
RIP my parents Mwenyezi Mungu awape Pumziko Jema,
Beautiful old days...daah sema tu maisha hayarudi nyuma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…