ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

ITV ilipofunguliwa mwaka 1994

Mortal kombat ITV 1999
IMG_0747.jpg
 
Nakumbuka enzi hizo nimemaliza la saba, tunaishi kurasini shimo la udongo. Mshua alikuwa tra alinunua hitach flani hivi mtaa mzima tv ilikuwepo kwetu tu. Na ilikuwa unailipia kila mwaka sijui kama ilivo bunduki.
Mmmh hii sikupata kusikia.
Au mlikuwa mnalipia Cable TV yaani huduma ya kupata matangazo ya TV stations kupitia cable?
TV kwa maana ya ile device sidhani kama iliwahi kulipiwa kwa mtindo huo.
Nasubiri majibu ya wengine.
 
Itv wanastahili kupewa super brand, maana ilifika wakati ikawa kama tv ya taifa kwa ubora wa muonekano na vipindi japo baadaye ikaja star tv na tvt. Kwa sasa itv bado iko vizuri ila hakuna mabadiliko makubwa kidigitali kama azam tv waliokuja kwa kasi ya ajabu kwenye soko la media. Azam kaongeza chaneli nyingi kuliko itv. Hata hivyo itv bado inatazamwa na watazamaji wengi wa taarifa ya habari
Kabla ya TVT na STAR TV kulikuwa na CTN, DTV na CHANEL TEN
 
Back
Top Bottom