Serikali ya Ivory Coast imevunja Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) baada ya malalamiko ya muda mrefu na kutoka kwa wapinzani kuhusu jinsi chombo hicho kinavyoendesha chaguzi nchini humo.
Hayo yamesemwa na msemaji wa serikali, Amadou Coulibaly, siku ya Jumatano. Coulibaly aliuambia mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha baraza la mawaziri kuwa uamuzi huo umeidhinishwa na serikali kufuatia mivutano ya mara kwa mara kuhusu uhuru wa tume hiyo na utendaji wake wa kazi wakati wa uchaguzi.
"Kutokana na mashaka yaliyoonyeshwa kuhusu taasisi hii (The Independent Electoral Commission, or CEI), pamoja na ukosoaji ambao imekuwa ikipokea, Baraza la Mawaziri limeamua kuivunja," alisema msemaji wa serikali na Waziri wa Mawasiliano, Amadou Coulibaly.
Aliongeza kusema, "Kwa sasa siwezi kusema mfumo mpya utakuwaje, lakini bila shaka utajadiliwa na kuwekwa sawa na serikali." Alibainisha kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kunakuwa na chaguzi za amani za kudumu kwa kujenga imani zaidi kwa raia wa Ivory Coast na wanasiasa wote.
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Pascal Affi N’Guessan, ambaye alizuiwa kugombea mwaka jana, ameitaka serikali kufungua milango ya mazungumzo na vyama vya siasa pamoja na asasi za kiraia ili kujenga upya mfumo wa uchaguzi kwa ajili ya amani na utulivu wa nchi.
Kwa muda mrefu, wapinzani wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa uhuru wa tume hiyo, ambayo ina jukumu la kuandaa chaguzi, kusimamia sheria za uchaguzi, na daftari la wapiga kura.
Mabadiliko ya katiba ya mwaka 2016 yalimwezesha Ouattara kugombea muhula wa tatu uliozua utata, uchaguzi ambao ulisusiwa kwa kiasi kikubwa na vyama vya upinzani.