Tuache ushabiki!! Hivi tunaweza kulinganisha utokaji wa Dr. Slaa na Lowassa kwenda CCM? Isitoshe, nimesema mwaka 2015 CHADEMA kulikuwa na mtu imara! Kukataa ukweli ni kutaka kuleta ushabiki usio na maana. Tusijisahaulishe uchaguzi mkuu wa 2010 Dr. Slaa ndie alipeperusha bendera ya CHADEMA, na alipata zaidi ya kura 2M. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2010, Dr. Slaa hakukata tamaa. Aakaendelea kukipigania chama, na kuzunguka huku na huko hadi dakika ya mwisho tulipomuona HAFAI na akaletewa Lowassa! Kwa kinyongo, Dr. Slaa akamwaga manyanga na kujiendea zake ughaibuni. Lakini hata huyo Lowassa, nae alijitahidi kuipambania CHADEMA pamoja na kuwa na matatizo ya kiafya, lakini kwavile shida yake ilikuwa urais tu, ndo maana alipoukosa, akarejea CCM.
Uhuni zaidi umefanywa na Membe.