Godfrey Constantine
New Member
- Aug 30, 2022
- 2
- 2
IWEKE DUNIA KUWA SEHEMU SALAMA NA SAHIHI YA KUISHI BINADAMU HATA KAMA HUNA DINI.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la makundi yanayotendeana wema na mazuri wao kwa wao ndani ya kundi lakini hawawezi kutenda wema huo nje ya kundi bali kutendea ubaya kundi lingine kwa maana wapo tofauti kiitikadi nao. Nao wakiamini kuwa hiyo ndiyo haki, usawa na ukweli. Mfano makundi makubwa ya kidini, nchi, ukanda, makabila. Makundi haya yamezua makundi madogo madogo ambayo yameleta mchafuko na kukosa tumaini katika jamii.
Makundi haya yamechangia ongezeko la ufisadi ,rushwa,ubinafsi,uhujumu uchumi,unyanyasaji ,kutesa watu,dhuruma kujilimbikia mali vyote hivi uchangia ongezeko la kukosekana kwa haki na umasikini duniani.
Chanzo kikuu kimetokana na viongozi ambao wana wajibu wa kuiongoza jamii yote na nchi katika njia bora na kupata maisha safi kwa kila mwanajamii lakini imekuwa ni kinyume viongozi wamekuwa wakijilimbikizia mali binafsi na makundi yao waliyomo, mbali zaidi huitumia dunia kama sehemu ya faida au kujinufaisha .
Mfano kuna kiongozi anaweza kumiliki zaidi ya bilioni 800 banki lakini nchi ina matatizo bado hawezi kuisaidia kwa chochote bali anatumia pesa zake kujilimbikia mali zaidi lakini si kutoa msaada, wakati pesa aliyonayo anaweza kutatulia matatizo ya inchi. Bali ujifanya nayeye anahali ngumu kama wao lakini katika hali hile hile matatizo yanapo zidi ukimbia inchi na kwenda mahali palipo na nafuu kwake.
Lakini kama angekuwa na imani ya uhakika ya kumcha MUNGU angekumbuka kuwa uongo, kuijilimbikizia mali ,ubinafsi havifundishwi kwenye imani zetu na MUNGU hafulaishwi navyo kabisa.
Ubinafsi mkubwa umejitokeza kati ya nchi na nchi ,unatokea pale inchi moja iwapo kwenye matatizo au balaa hawa hawa viongozi wakosa imani hata kama ni majirani huyatumia matatizo ya mwezio kama sehemu ya kujilimbikizia mali au huyafanya matatizo ya wenzao kuwa sehemu ya faida. Mafano, tunoana nchi inatumika kuwasaidia wahasi wa nchi moja kama sehemu ya kusafirishia silaha za kivita na kambi za waasi, pia maficho pale wanapozidiwa. Binadamu hatakiwi kusahau kuwa kuna dhana ya msambao wa tabia jambo laweza kutokea sehemu ndogo ya dunia muda likaikumba dunia nzima, tukumbuke msambao wa Corona.
Balaa la njaa lina potokea mipaka ya nchi na nchi ufungwa kila nchi ikilinda watu wake lakini nchi moja inaweza ikawa na chakula cha kutosha lakini ikafunga mipaka yake na kuwauzia majilani zake chakula kwa gharama ya juu huku ikiendelea kuyaona matatizo ya nchi hiyo kuwa ya kwao pekeyao. Pia kwenye matatizo mipaka kutoka nchi moja kwenda nyingine imekuwa inavizuizi vikubwa mno nibora watu wafe lakini ruhusa ya kuvuka mipaka hawapati bila kusahau jamii za mipakani zinamwingiliano na mahusiano makubwa kati ya nchi na nchi(undugu).
Viogozi hawa wamepelekea mataifa mengi kuwa na roho mbaya na ubinafsi uliokisili ambao upelekea kuanza kuligawanya taifa lao pia,hivo wao kwa wao kugawanywa kikanda ,kimikoa ,kidini na kimakabila.kunaanza kwa matambishiano na kubaguana vitu vyao kwa pande moja na nyingine. Mfano tunaona nchi inaweza kuwa na machafoko upande fulani wa nchi lakini nchi hiyo ikaona kama upende ule watalitatua tatizo lao kwa ukanda huohuo bila kuwasaidia ukanda hule na upelekea kubadilika na kuwa sehemu mbaya zaidi (bad zone) lakini upande mmoja uona kama ndio tabia yao na kuutumia ukanda hule kama sehemu ya kufanyia biashara haramu na yakujipatia faida.
Ikumbukwe viongozi wanchi ndio waliokabiziwa mamlaka kutoka kwa mwenyezi MUNGU kwa mjibu wa dini zetu ,kwa kuongoza watu kwa haki na amani. Huku wakishirikiana na viongozi wa dini,Ili kutenda haki na usawa kwa makundi mbalimbali kama vile watoto ,vilema ,wazee ,wanawake na watu wenye magonjwa ya aina mbali mbali iliwapate tumaini la kuendelea na maisha, na pia kuyafulahia maisha ya nchi yao lakini watu hawa uifanya nchi kama mali yao ya kujipatia faida na kusahau mstakabari wa maisha ya watu wengine wamekuwa hawana malengo ya nchi yao bali wana malengo yao binafsi. Mfano tangia nchi za kiaafrika zianze kupata uhuru kumekuwa na uhaibikaji wa viongozi pale wanapo chunguzwa baada ya kumaliza muda wa uongozi au kufariki wanakutwa na mali nyingi ambazo wameficha kwenye akaunti za siri nje ya nchi.Hii hujenga kutoaminiana ndani ya nchi na kuondoa umoja na mshikamano katika maisha yajayo ata sasa ,ambapo tunaona nchi nyingi zinazo endelea viongozi wake wanakumbwa na kashifa hizi.
Lahana ya viongozi hawa inajipandikiza kutoka kizazi hadi kizazi kingine sehemu hadi sehemuna. Hapa matendo ya ufisadi ,dhuruma ,unyanga’anyi, kujilimbikizia mali ya naanza kuonekana katika familia na watu ndani ya nyumba moja(kaya). Kila mtu anakuwa na tabia mbovu lakini ikifulaiwa tu na familia. Mfano tunaona nchi ya Afrika Kusini imekuwa na tabia mbaya ya watu wake lakini watu wemesahau kuwa tabia hii imejengwa na viongozi wa taifa hilo kukosa kuwaongoza watu katika njia nzuri, walianza kuwafanyia wageni na sasa wameamia wao kwa wao kuanza kufanyiana vitendo viovu.
Viongozi wakubwa wa dini nao wamefuata tabia ya watawala wao na kusahau wajibu wao hivyo wamekuwa wakifanya maombezi ya kupata mali kwa uraisi na kuwatetea viongozi ata kama wakifanya vitendo vya kumchukiza MUNGU. Pia nao wamejikita katika kujilimbikizia mali na sio kuishauri Serikali au kuwaosaidia jamii ya taifa husika. Mfano hawaikosoi Serikali au kuisaidia kimawazo kuhusu hali ya watu wake bali huungana nayo hata kwenye uhalifu. Mfano tunaona vikudi vya baazi ya viongozi wa dini wanausika na kuwaunga mkono wahasi na vikundi vya kiuharifu.
Tabia ya watu katika nchi fulani inachochewa na tabia ya viongozi wao kwani wao wakiwa safi na jamii itakuwa safi lakini si hivyo kumekuwa na viongozi waongo na wasaliti kwa jamii zao hivyo imechangia watu wanchi kuwa hawana tumaini lolote la maisha na mstakabali wa maisha yao ya baadae hivyo watu wanaona ni bora kutumia njia zozote kupata fedha na mali kwa sababu sheria ya nchi ipo kwa kuwalinda watu wachache ambao ni viongozi ndani ya nchi na wakuu wa makundi mbalimbali.
Maambukizi ya tabia mbaya yamekuwa yakiigwa kwa kasi zaidi kutokana na kasi ya kukua utandawazi na upungufu wa imani ya kumcha mungu. Watu huyachukua matendo maovu kama sehemu ya mbinu na ujanja wa kujinufaisha lakini kumbe ndio kupotea kwenyewe. Watu wanatumia utandawazi kuiga mbinu mbalimbali za kujinufaisha wao binafsi kwa sababu njia hizo ni siri na chafu hawawezi kuzianika hazarani au utafuta namna ya kuishawishi serikali isiyo kuwa na imani ya MUNGU kuzipitisha na kuhararisha ziwe sehemu ya maisha ya watu wake mfano tumeona haki ya wapenzi wa jinsia moja.
Kabla hakujashindikana kila sehemu na ongezeko kubwa la watu wafanyao maovu na kuyageuza kama sehemu yao ya maisha ya kila siku dunia. Nchi moja moja zinatakiwa kupandikiza chembe za imani ya kumcha MUNGU kwa vizazi vijavyo ili kupunguza au kuzuia dhiki na tabu itakayoikumba dunia ,kwani tukisema yalioandikwa lazima yatimie basi vitendo vya kuielimisha jamii na kupunguza maozo ya jamii tutakuwa tunadanganyana na kuichelewesha dunia ya wharifu. Dunia kama meli yenye tundu ,inazibika au hazibiki?hilo ni swali ambalo jibu lake litaipa dunia mwelekeo.
Angalizo la nchi na dunia kwa ujumla ni kwamba kutazuka sehemu ambazo hazitawaliki na wala haziongozeki, wimbi kumbwa la wakimbiaji matatizo wakizani sehemu fulani ni nafuu ,angezeko la vitendo vichafu, makundi makubwa ya kiuharifu hili mladi watu wapate fedha za kuishi, na hata wenye roho safi nao watabadilika ili waweze kuishi kwani bila kufanya hivyo niraisi kutangulia kufa. Kutakuwa na sehemu mbaya za kiishi nyingi(bad land) ambazo hata vyombo vya dola vyenye dhamana ya kulinda watu vitashindwa kuzuia hali hiyo na kuungana na makundi ya wahalifu. Fedha itakuwa ndio kila kitu na hata mafundisho ya dini yatabadirika yatakuwa ni katika kutafuta pesa tu na sio mkatazo halisi ya neno la Mungu.
JE, BINADAMU ANATEKELEZA YALIYOANDIKWA PASIPO KUJUA AU ELIMU YAKE ITAMSAIKIA KUTENGUA YALIYOTABIRIWA.
Mwandishi,
Godfrey Masanja,
0762460956,
ileje.

Upvote
0