Iwekwe siku ya kumbukumbu na kuenzi mchango wa Muziki wa Dansi katika kukuza lugha ya Kiswahili

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Katika kumbukumbu za siku ya kiswahili, sijawahi kusikia wakitajwa wasanii wa Muziki wa Dansi katika kukuza lugha ya kiswahili hasa wakati ule ambapo jamii nyingi zilikuwa Bado hazijafunguka na wengi walisthiriwa na vilugha vyao.

Lakini wanamuziki wa enzi hizo kwa majitoleo na uzalendo mkubwa walijitahidi kutumia kiswahili katika utunzi wa nyimbo zao, na walikwenda kujitoa na kuburudisha jamii Huku wakieneza lugha yetu ya Kiswahili kwa nini tunasahau hili kitu muhimu
 
Na kumbukumbu hiyo iende sambamba na kumuenzi nguli, mwanamuziki bora wa dansi kuwahi kutokea nchini Banza Stone.
 
Hakika na wengine wako wengi, Marijani Rajab u, mbaraka mwinshe, Patric Balisidya, Ndala Kasheba, Ali Zahir Zoro, Maestro King Kiki na wengine kama Dr. Remmy Ongala.
 
Katika kumbukumbu za siku ya kiswahili, sijawahi kusikia wakitajwa wasanii wa Muziki wa Dansi katika kukuza lugha ya kiswahili hasa wakati ule ambapo jamii nyingi zilikuwa Bado hazijafunguka na wengi walisthiriwa na vilugha vyao.

Lakini wanamuziki wa enzi hizo kwa majitoleo na uzalendo mkubwa walijitahidi kutumia kiswahili katika utunzi wa nyimbo zao, na walikwenda kujitoa na kuburudisha jamii Huku wakieneza lugha yetu ya Kiswahili kwa nini tunasahau hili kitu muhimu
Uko sahihi kabisa wanamziki wa dansi
  1. Waliimba kwa kiswahili fasaha
  2. Muziki ulilenga kuijenga jamii kimaadili
  3. Muziki wao ulibeba ubunifu na ufundi wa kupiga vyombo vizuri kabisa
  4. Muziki wao ulikuwa na mvuto
 
Tuungane wote tupige campaign MwanaFA alishupalie tumtag walijue hili.
 
atakuja mtu wa taarabu nae atataka iweke siku ya taarabu pia
 
Nasikiliza TUMA hapa ya ottu jazz(msondo ngoma) naburudika kweli kweli.
 
Back
Top Bottom