MBEBA MAONO KAJA
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 365
- 195
Wanajamvi kama heading inavojieleza,
Katika vitu huwa nakosa tafsiri sawia, ni suala zima la mapenzi yaani kuanguka penzini. Kweli usipofikiwa na hali ya kupenda au kumpenda mtu inakuwa hivi; Mtu akikueleza jinsi alivoanguka penzini au ukimuona na kumsikia mtu aloanguka penzini hata hajielewi,unakuwa mwepesi kumtolea ushauri kama vile unamuona kapotea.
Jamani mapenzi yanatafsiri sahihi kwa mhusika tu. Hii misemo ya penzi kama haijakufika,utaongea lolote,au mtu akija anaomba ushauri juu ya mwenendo wa kipenzi chake, kiukweli utamuona huyu vipi si aachane nae tu.
Jamani sio rahisi kukiacha kitu unapenda, upendo ni kama upofu wakati mwingine bora upofu.
Naomba nikiri humu ndani mimi ni miongoni waliokuwa hawaamini kuwa mtu ulokutana nae ukiwa una meno thelathini na mbili anaweza kukufanya umuwaze na ukimkosa kwa lolote uugue, niliijenga imani kuwa siwezi na sitoweza kumpenda mwanamume kiasi hicho kinyume chake.
Hadi nimeamua kuandika humu ndani ingawa ni member huwa sichangiagi sana ni vile huyu mwanamume mkarimu alivonipagawisha. Ni mwanamume anaejitambua miongoni mwa wote nilokutana nao. Asante kwa upendo wako pia.
Huyu mwanamume nampenda to the maximum.
Najiona Maneno yangu ni machache kuelezea vile nampenda. My words are too shallow to express my loving impressions to you JFM.Yamkini umeambiwa mengi na ulowahi kuwa nao kabla yangu, naomba J uchukulie kuwa hii ni aina ya pekee ya upendo nilonao kwako. Huyu mwanamume kweli kama ni Mwenyezi Mungu kaniletea basi sina budi kutoa shukrani zangu kwake, maana anatosheleza niloyatafuta kwa mwanamume wa maisha yangu kipindi kirefu. J popote ulipo humu ndani najua wewe ni expert member hapa, ninamaanisha hiki nilichokiandika.
Wanajamvi mimi na huyu wangu hatujakutana humu ingawa wote ni member wa humu.
Nakupenda sana. Mungu atujaalie tufikishe malengo yetu.